Ufugaji wa Sungura Tanzania

Ufugaji wa sungura kwa Tanzania ni ufugaji unaokuja kwa kasi kwasababu ufugaji bora wa sungura husaidia sana kuongeza kipato kwa wafugaji.

Ufugaji huu bado haujakuwa maarufu kwa wafugaji wengi na hupedelewa kufugwa kwa mapenzi au mapambo tu ya mfugaji na siyo kama shughuli ya kuingiza kipato.

Lakini iwapo wanyama hawa watafugwa katika mazingira ya usafi na kulishwa vizuri huweza kukua haraka na kumpatia tija kubwa mfugaji.

Aina za Sungura Wafugwao

Kuna aina mbalimbali ya sungura ulimwenguni, lakini hapa Afrika Mashariki aina tatu ndiyo maarufu na hupendwa wengi.

Aina hizo ni California white, New Zealand White na Flemish Giant.

  1. California White

 Kabila hili huwa na rangi nyeupe na nyeusi kwenye pua,masikio na mkiani (kama inavyoonekana pichani). Huweza kuku na kufikka kilo 7 hadi 8.

Kama watapatiwa nafasi ya kutosha, huweza kuzaa mara nne kwa mwaka na huzaa hadi watoto 8 kwa kila mzao.

  1. New Zealand White

 Sungura wa kabila hili huwa na rangi nyeupe tu. Hukua na hata kuweza kufikia kilo 8. Iwapo watapatiwa nafasi na chakula bora cha kutosha huzaa mara nne. Na huzaa watoto 7 hadi 15 kwa kila mzao.

  1. Flemish Giant

Hawa huwa na rangi ya kijivu na wengine huwa na rangi ya kibluu iliyochanganyika na nyeusi. Hukua na kufikia kilo 6.

Lakini wanapopandishwa na makabila mengine hapo juu basi watoto (kizazi) chao huwa na ukubwa na uzito zaidi kuliko wazazi.

Faida za Ufugaji wa Sungura

  1. Nyama

siyo faida pekee ya ufugaji wa sungura: japokuwa faida kubwa ya ufugaji huu ni nyama, bado ulaji wa nyama ya sungura siyo maarufu nchini kama ilivyo sehemu nyingine ulimwenguni.

Hata hivyo kuna ushahidi wa kitafiti unaonyesha kwamba hivi sasa kuna baadhi ya hoteli nchini huoendelea zaidi nyama ya sungura kuliko kuku.

  1. Mikojo

Mikojo ya wanyama hawa huwa na kemikali za ammonia na uric acid. Mkojo huu huweza kuchachuliwa (diluted) na maji kwa uwiano wa 1:7 na kutumiwa kama dawa ya kudhibiti ukungu (fungicide) kwenye mimea mashambani.

Mkojo pia unaweza kutumia kama kirutubisho cha majani kwenye mmea kwa kuwa na kemikali ya ammonia.

  1. Samadi

Samadi itokanayo na mnyama huyu huwa na wingi wa madini ya Nitrogeni na Phosphorus ambazo licha ya kuwa ni virubisho muhimu vya ardhi pia husaidia kudhibiti mashambulizi kwenye mimea yanayosababishwa na wadudu na bakteria wa aina mbalimbali.

Faida Nyingine za Ufugaji wa Sungura

  1. Ni rahisi kufuga
  2. Ni rahisi kuwalisha
  3. Huzaliana kwa haraka na wanakua tayari kuchinjwa na kuliwa baada ya miezi 4 tu.

Faida za Nyama Ya Sungura

  1. Nyama ya sungura haina mafuta (fats) wala lehemu (cholesterol)
  2. Ina kiwango kikubwa cha protini kuliko nyama zitokanazo na aina zote za mifugo tunayoifuga
  3. Miili yao huwa na nyama zaidi kuliko kuku wa uzito unaolingana
  4. Nyama ya sungura ni laini huiva kwa muda mfupi inapopikwa

Mambo Ya Kuzingatia Kwenye ufugaji wa Sungura

  1. Sungura Wapewe Chakula

Sungura wanahitaji kupewa vyakula vilivyokatwakatwa vipande (pellets) au aina nyingine za mlo ambao utaweza kuwatosheleza kutwa nzima.

Kuna vyakula vichache ambavyo kwa kawaida hawapendelei maganda ya karoti, viazi ulaya lakini hupendelea sana malisho kama vile Napier grass na Lucerne.

Malisho ya majani wanaweza kupewa lakini kwa kiasi kidogo.

  1. Sungura Wapewe Maji

Wapatiwe maji ya kutosha licha ya ukweli kwamba vyakula wanavyokula huwa na majimaji lakini bado miili yao huitaji kiasi kikubwa cha maji.

  1. Vyombo Vya chakula Viwe Vizito

Vyombo vya malishio au manywesheo visimikwe vizuri ardhini au viwe vizito ili kupunguza uwezekano wa kuangushwa na sungura.

Vilevile inashauriwa kuwaongezea madini kama Farmers Superlick kwenye malisho yao. Madini haya husambazwa na Makampuni ya Farmers Centre na Farmbase na wakala wao mikoani.

Ujenzi wa Banda Zuri La Sungura

  1. Ujenzi wa Banda la Sungura

Banda liwe limeinuka kiasi cha sentimeta 90 toka ardhini pia liwe na kimo cha sentimeta 90 na upana wa sentimeta 90.

Kwa vile mabati mengi huwa na ukubwa wa mita 2.5 hivyo inakuwa busara kuwa na mabanda ya upana wa sentimeta 90 ambapo mabanda mawili yataweza kufunikwa na bati moja tu la ukubwa huo.

  1. Ujenzi wa Sakafu Ya Sungura

Upande wa sakafu banda lifunikwe kwa waya (tazama picha chini) ili kuwezesha kinyesi na mikojo kuondoka kwa urahisi

Weka tabaka la majani makavu (hei) kwenye matandazo, kwani hii ni sehemu muhimu ya malisho ya sungura na itasaidia kuwapatia malisho hasa wakati wa usiku.

  1. Usafi wa Banda La Sungura

Mabanda ya sungura yasafishwe kila siku na matandazo yaliyochafuliwa kwa mikojo, vinyesi au majimaji yaondolewe mara moja.

Yanaweza kutumiwa kama virutubisho vya udongo bustanini na matandazo mapya yarejeshwe, hii itasaidia kuwaweka sungura wako katika hali ya usafi pia kutaepusha inzi ambao husababisha milipuko ya magonjwa

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

2 Comments
  1. Nimejifunza Mambo mengi sana kwa kusoma habari za ufugaji wa kuku, Bata na sungura. Kwa Sasa nafuga kuku takribani hamsini ila natamani kuwa mfugaji mkubwa wa Bata, kuku na sungura.

  2. Nataka kufuga sungura sijui mbegu inapatikana wapi

Leave a reply