About Me

Najua unatamani kufahamu Mimi ni nani na pia nina Ujuzi gani kichwani. Mimi naitwa Lenald Minja naishi Dar es salaam.

Unapata Changamoto Gani Mtandaoni?

Mtandaoni Kunahitaji Uvumilivu sana Kwasababu Mpaka leo hii nimesha fanyaga project nyingi sana za mtandaoni na nimepitia changamoto nyingi sana na mwisho wake zote zikafa.

Mfano hata Hii website ya Wauzaji.com kipindi cha nyuma nilikuwa nimeitengeneza kwa kutumia code zangu mwenyewe.

Baadae nikafanya uzembe mdogo wa kiusalama matokeo yake ikadukuliwa ikanibidi nianzishe upya kwa kutumia namna nyingine.

Umesomea Elimu Gani Darasani?

 1. Confirmation – Kipaimara (2 Years)
 2. Mechanics – (2 Years)
 3. information Technology (3 Years)

Umesomea Elimu Gani Mtandaoni?

 1. Search engine optimization
 2. Computer user support
 3. Hardware troubleshooting
 4. Software troubleshooting
 5. interpersonal relationship
 6. Cctv system operating
 7. Cms website designing

Umesomea Ujuzi Gani Mwingine?

 1. Driving Skill – Daraja A, A2, B na D

Unapenda Vitu Gani Kwenye Maisha?

 1. Napenda kuwasaidia watu

Kutokana na kusoma na kupenda sana maswala ya Teknolojia nimekuwa najikuta napenda sana kuwasaidia watu kwenye mambo yanayohusiana na teknolojia na mawasiliano.

 1. Napenda kufanya mazoezi

Kutokana na kutambua ya kuwa afya njema inachangia sana utendaji mzuri wa kazi hivyo nimejikuta napenda sana kufanya mazoezi ili kulinda afya yangu kwa ujumla.

 1. Napenda kusikiliza muziki

Binafsi napenda sana kusikiliza muziki kwa sababu muziki umekuwa unaniburudisha sana endapo nikiwa nimechoka kimwili au kiakili.

Unachukia Vitu Gani Kwenye Maisha?

 1. Sipendi mwenzangu ashindwe

Najisikiaga sana vibaya endapo nikiona mtu anapata changamoto katika utumiaji wa Teknolojia kwasababu mimi ninao uwezo wa kumuelekeza tena kwa ufasaha.

 1. Sipendi kuikwepa teknolojia

Kutokana na Teknolojia kurahisisha mambo najiskikiaga vibaya sana kuona mtu anakuwa nyuma kwenye utumiaji wa Teknolojia kutokana na kuto kuielewa kwa Ufasaha.

 1. Sipendi kupewa sifa

Kufanya Kazi kwa usiri, juhudi, maarifa, uaminifu na kujituma bila kuamrishwa huo ni wajibu wangu hivyo basi sipendagi kuona mtu ananisifia katika hayo mambo.

Mawasiliano Yangu

Kama unataka kuwasiliana na mimi nakuomba unitumie email.

Email Yangu Binafsi [email protected]

Wauzaji
Logo