About Wauzaji

Mtu aliyeandika hapa ni mimi mwenyewe Lenald Minja muanzilishi wa hii website. ukitaka kunijua kiundani zaidi bonyeza hapa “About Me“.

Kwanini Nimefika Hapa?

Hata mimi mwenyewe ndio najiuliza umefikaje hapa Aisee ila nahisi kuna sehemu umebonyeza pameandikwa About Us ndio ukaletwa hapa.

Kwani Wauzaji Mnauza Bidhaa?

Hapana, Humu ndani ya wauzaji hakuna bidhaa inayouzwa humu ni utakutana na list ya wauzaji wa jumla ambao wamesajiliwa na waaminifu.

Kwahiyo Sasa Wauzaji inatatua Tatizo Gani?

Wauzaji inawasaidia wanunuzi walio ndani na nnje ya Tanzania kuwapata wauzaji na wasambazaji wastaharabu na wanao chapa kazi kwa juhudi.

Kwanini Wauzaji inatumia Kiswahili?

Kwenye website yote ya wauzaji imetumika lugha ya kiswahili ili hata yule binamu yako asiyejua kabisa kingereza aweze kuelewa kwa haraka.

Hapo juu nilikuwa natania Aisee kwanza najua kwenu wote kizungu kinapanda. Jibu ni kwasababu nimeona wauzaji ikitumia kiswahili tutaelewana vizuri.

Kwani Wauzaji inahusiana na Nini?

Website ya wauzaji ndani yake inahusiana na mambo mbalimbali ila Kwa ujumla asilimia kubwa ya mtandao wa wauzaji unahusiana na;

  • Orodha ya wauzaji
  • Review za wauzaji
  • Maelezo ya biashara
  • Maelezo ya ufugaji
  • Maelezo ya kilimo
  • Maelezo ya maisha

Kwani Wauzaji ina Watembeleaji Wangapi?

  • Daily visits: 2,000+
  • Daily pageviews: 3,000+
  • Monthly pageviews: 90,000+ (85% Organics)
  • Email list: 6,500+

Tuna update hizi taarifa kila baada ya miezi mitatu ziweze kuendana na uhalisia wa kupanda na kushuka kwa idadi ya watembeleaji.

Mawasiliano Yangu

Kama unataka kuwasiliana na mimi nakuomba unitumie email.

Email Yangu Binafsi [email protected]

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general