Ufugaji Bora wa Nguruwe Dume wa Mbegu

Ufugaji wa nguruwe dume wa mbegu mara nyingi hutegemea na aina ya makundi ya nguruwe na aina ya mfumo wa ufugaji wa nguruwe ambao umepanga kuutumia katika ufugaji wako.

Makundi ya nguruwe ni kama vile madume ya mbegu, majike wazazi, watoto, na wale wanaonenepeshwa kwa ajili ya nyama au mafuta.

Unaweza kufanya ufugaji wa nguruwe ndani au nje ya banda kutegemea na ukubwa wa shamba, kipato kilichopo kwa shughuli za ufugaji.

ili kuleta mafanikio na tija katika ufugaji wa nguruwe ni vema kuzingatia utunzaji bora ikiwa ni pamoja na aina ya banda, uchaguzi wa nguruwe wazazi, ulishaji, udhibiti wa magonjwa na uangalizi kwa ujumla.

Mambo ya kuzingatia katika ufugaji wa nguruwe dume

1. Uchaguzi WA nguruwe dume bora

Wakati wa kuchagua mbegu bora ya nguruwe mfugaji anashauriwa kuzingatia yafuatayo ;

 • Achaguliwe kutoka kwenye koo wenye historia ya kukua haraka, kukuza watoto wengi na kuwatunza, kutokuwa na magonjwa au kilema cha kurithi.
 • Awe na miguu imara, mchangamfu na mwenye afya bora
 • Awe na umbile zuri linaloendana na aina yake na misuli imara itakayomwezesha kupanda bila matatizo
 • Awe na kende mbili, kubwa, zilizokamilika na zinazolingana
 • Awe anayekua haraka na mwenye uwezekano mkubwa wa kumfanya kuwa kitowewo
 • Awe na chuchu zisizopungua 12
 • Asiwe na mahusiano ya kinasaba (kama kaka na dada, mtoto na mama au mtoto na baba) na majike anayotegemea kuyapanda
 • Awe mrefu na mgongo ulionyooka
2. Ulishaji wa nguruwe dume

Dume kwa ajili ya kupandisha apewe chakula bora chenye viini lishe vya kutosha vitakavyotosheleza mahitaji ya mwili bila kumfanya mnene sana au kukonda. Wakati wa msimu wa upandishaji alishwe chakula bora kiasi cha kilo 2.7 hadi 3.6 kwa siku.

Wakati ambao sio msimu wa kupandisha, dume apewe chakula bora kiasi cha kilo 2 kwa siku. Kwa matumizi mazuri ya chakula hicho kigawanywe na kulishwa mara mbili kwa siku.

Pia inatakiwa dume apewe maji safi na salama ya kutosha kila siku wakati wote.

3. Kinga ya magonjwa ya nguruwe
 • Katika ufugaji wa nguruwe Uzuiaji wa magonjwa na wadudu ni muhimu kwa afya ya nguruwe dume. Mfugaji anashauriwa kumwona mtaalam wa mifugo aliyekaribu nae ili kupata ushauri juu ya ufugaji wa nguruwe ikiwemo chanjo muhimu kwa ajili kuzuia magonjwa kwa wanyama wake.
  • Mfano kwenye sehemu ambazo ndorobo, mfugaji anashauriwa kutumia chanjo.
 • Kuzuia wadudu, mfugaji anashauriwa kuogesha nguruwe kwa dawa za kuogeshea angalau mara mbili kwa wiki ili kuzuia ukurutu na matatizo mengine ya ngozi.

Kuzuia minyoo mfugaji anashauriwa kuwapa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu. Ni muhimu banda, vifaa vya kulishia na kunyweshea maji viwe safi wakati wote.

Jinsi ya kupandisha nguruwe dume

Upandishaji wa nguruwe unaweza kufanyika kwa njia mbili, ya KUTUMIA DUME au UHAMISHAJI. Njia ya kutumia dume ndio inayotumiaka hapa nchini kwa utaratibu ufuatao ;

 • Nguruwe dume aruhusiwe kupanda kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miezi nane hadi kumi
 • Akiwa na umri wa miezi 10 hadi 18 anaruhusiwa kupanda mara moja kwa wiki
 • Akiwa na miezi 18 hadi 24 anaruhusiwa kupanda mara nne hadi tano kwa wiki
 • Dume wakubwa wasitumike kupanda majike wadogo kwani wanaweza kuleta madhara kama vile kuwavunja migongo.
 • Dume aruhusiwe kuendelea kupanda mpaka umri wa miaka 5 hadi 6

Katika ufugaji wa nguruwe inashauriwa kuwa ni muhimu dume la kupandisha liwekwe kwenye chumba chenye eneo la mita za eneo 9.3 ili kuweza kupata mazoezi ya mwili ikiwa sehemu ya kupanda imetenganishwa eneo liwe la mita mraba saba. Madume yatenganishwe na Majike ili kuepusha kupanda wakati usiotakiwa.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

4 Comments
 1. Mimi ni mfugaji wa nguruwe na mifugo wengine kama kuku na samaki. Napenda kuwa shukuru sana kwa elimu ya ufugaji wa nguruwe niliyoipata kutoka kwenu.

  Na pia ningeomba kama kuna uwezekano wa kunipa support juu ya uuzaji wa nguruwe kupitia website yenu ya wauzaji mtakuwa mmenisaidia sana Asanteni.

  • Asante sana Tunashukuru Kwa Kuonesha Kupendezwa na Elimu yetu.

   Kuhusu Swala la Kuungana na Sisi Wauzaji linawezekana ila Tu Uwezekano wa Kukubaliwa Sio Mkubwa Sana Kutokana idadi Ya Watu Wanaohitaji ni Wengi.

 2. Asante sana nimepata elimu ya kutosha kuhusu ufugaji bora wa nguruwe ila tatizo linakuja kwenye masoko naomba msaada kwa Hilo.

Leave a reply