Mbinu za Jinsi Ya Kufanikiwa Katika Biashara Tanzania

Jinsi ya kufanikiwa katika biashara tanzania na mbinu ambazo zitapelekea kupata mafanikio katika kuendesha na kukuza biashara yako ukiwa tanzania

1. Katika Biashara Uza Bidhaa Zenye mashiko

Kupata wateja kwenye biashara yako unatakiwa kuwa na kile wanachohitaji. Huwezi kuuza mwavuli msimu ya jua kali kwani hakuna atakayenunua.

Kama mfanyabiashara, ni muhimu kusoma soko lako siku zote na kuwapatia wateja kile wanachohitaji na sio vinginenyo. Ukiwa na biashara yenye bidhaa ambayo uhitaji wake kwenye soko ni mkubwa lazima watu wanunue.

2. Bei za Bidhaa zako ziendane na Uhalisia

Baadhi ya wafanyabiashara wamejikuta wakidorora kutokana na maamuzi yao ya kuuza bidhaa kwa gharama kubwa ambayo asilimia kubwa ya wateja wanashindwa kumudu. Wakati unapangilia bei ya bidhaa katika biashara yako ni vizuri kuweka akilini nani hasa ni soko lako.

Jiulize katika mazingira uliopo utapata wateja wangapi kwa bei hiyo Hakuna mtu atakayetumia kiasi kikubwa cha fedha kupata bidhaa ambayo wafanyabiashara wengine wanauza kwa bei rahisi zaidi.

3. Kuwa Mpambanaji Katika Biashara Yako

Kama unamiliki biashara au unafikiria kuanzisha biashara hupaswi kuwa mzembe Unatakiwa kuwa tayari kutoa huduma bora kwa wateja wako muda wote.

Kuwa tayari kumshauri mteja kumuelekeza pale ambapo anapata wakati mgumu kuelewa na kuwa mtu ambaye ambaye yupo tayari kutoa msaada kwa wateja wake pale wanapohitaji. Usiwe mfanyabiashara ambaye anakaa tu dukani akitegemea wateja watamfuata pasipo ushawishi wowote.

4. Geuza Wateja Kuwa Marafiki Katika Biashara

Kujenga mahusiano kwenye biashara kimsingi yatakufaidisha wewe. Ukiwa na wateja wa muda mrefu kwenye biashara yako basi wateja hao hugeuka kuwa marafiki.

Uaminifu wao kwenye bidhaa na huduma zako utawafanya warudi kwako mara zote pale wanapohitaji kitu.

Hili ni jambo zuri kwa mfanyabiashara kwani ni uwanja mzuri wa kupanua soko. Unaweza kuwaomba wateja hao watangaze biashara yako kwa marafiki zao kupitia mitandao ya kijamii na hata wanapokuwa nyumbani.

5. Usikate Tamaa Katika Biashara

Kuna wakati mambo yatakuwa magumu katika biashara na Mipango yako haitoenda kama unavyotaka na hali hii huenda ikakuvunja moyo na kukufanya ukose motisha ya kufanya kazi kwa bidii.

Hutakiwi kukata tamaa kwenye biashara yako jitahidi kujifunza kutokana na makosa pia omba ushauri kutoka kwa wafanyabiashara wenngine au hata wataalamu.

Changamoto mbalimbali ambazo zipo kwenye shughuli zako zisikuvunje moyo. Endelea kujituma na baada ya muda mambo yote yataenda sawa.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

4 Comments
  1. Asante sana Pia nilikuwa naomba mnisaidie namna ya kupata wateja wengi katika biashara mpya kwa hapa Tanzania.

  2. Hata mimi kwenye mbinu zangu za biashara najitahidi sana Kuhakikisha nakuwa na huduma nzuri kwa wateja.

Leave a reply

Wauzaji
Logo