Faida Ya Kulipia Matangazo Kwenye Facebook

Faida Ya Kulipia Matangazo Facebook?

Facebook Sponsored Ads inatoa matokeo bora hasa kwenye kutangaza biashara yako au huduma yako kuliko njia nyingine yeyote.

  • Unaweza kutangaza biashara au huduma yako kwenye eneo husika

Unapofanya matangazo ya Sponsored mara zote inakupa chaguzi ya kuchagua wapi unataka kuwatangazia biashara au huduma yako.

Mfano unaweza kuamua kutangaza biashara kwa eneo lote la Tanzanaia au kutangaza katika wilaya moja wapo nchini.

Hii inakupa faida ya kuwa na wateja ambao ni walengwa kwenye biashara yako kwa sababu watu uliowalenga wanapatika katika eneo ambalo wewe umelilenga kama eneo lako la kibiashara.

  • Unaweza kuchagua Umri wa wateja wako

Kuna baadhi ya biashara huwa zinazingatia umri wa wateja, mfano kama unafanya biashara ya vinywaji ambavyo ni vilevi ni wazi kuwa unahitaji watu wenye umri usiopungua miaka 18.

Kwa kutumia Facebook Sponsored Ads unaweza ukachambua umri wa wateja wako kwa urahisi ili kupata wateja halisi.

  • Unaweza kuchagua Jinsia unayoilenga

Kuna biashara zinazingatia jinsi Kuna biashara ambazo wateja wake maalumu ni wa jinsia ya kike lakini zipo biashara ambazo wateja wake maalum ni jinsia ya kiume.

Unapotumia Sponsored Ads inakupa uwezo wa kutangaza biashara yako kwa wateja ambao ni walengwa.

  • Unaweza Ukachagua Lugha

Lugha ni kigezo kikubwa katika biashara Na ndio ni njia ya mawasiliano kwenye biashara yeyote Unapofanya matangazo ya biashara yeyote kwanza lazima ujue nani unamlenga kwenye baishara yako.

Facebook Sponsored Ads itakupa chaguzi ya lugha ambayo ndio njia pekee ya mawasiliano kati yako na mteja wako.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

2 Comments
  1. Namependa sana faida hii ya Huduma ya kulipia matangazo facebook Asante sana.

Leave a reply