Ufugaji wa Samaki Tanzania

Ufugaji wa samaki kwa Tanzania ni mzuri sana na pia huleta kipato kwa wafugaji wa samaki na Tanzania Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi wafugwao.

Samaki wapo wa maji baridi na wa maji chumvi.

Mahitaji Ya Ufugaji wa Samaki

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi, maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.

Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa liwe. Bwawa linaweza kuwa la kujenga kwa kutumia saruji (cement), kutandika nailoni (plastic) au la kuchimba tu.

Bwawa huchimbwa au kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi.

Aina za Samaki Wanaofugwa Zaidi

Kuna aina nyingi zaidi za samaki wafugwao katika maeneo mbalimbali hapa nchini, na duniani kwa ujumla. Miongoni mwa samaki hao ni pamoja na Sato, Kambale na aina nyinginezo ambazo hufugwa kwa wingi zaidi.

Kiwango Cha Samaki Kwa Eneo

Ili kuwa na ufanisi, unahitaji samaki 7-8 katika mita moja ya mraba. Hii ina maanisha kwamba kama una mita za mraba 600, basi unaweza kufuga samaki 4,500.

Haishauriwi kurundika samaki kwenye eneo ndogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa safi ya oxygen.

Jinsi Ya Kufanya Bwawa Liwe na Hewa

Zipo njia nyingi za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa. Ukishachimba bwawa, (aidha na kulijengea), ingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa.

Ni lazima kumwagia chokaa kwenye bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua vimelea kama bakteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako.

Unahitajikaka pia kurutubisha maji hayo kwa kuchanganya na mbolea.

Unaweza kutumia mbolea kama ya ng’ombe na mbolea za viwandani, ingawa haishauriwi sana kutumia mbolea za viwandani.

Baada ya kutumia mbolea inashauriwa kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi. Hii ni kwa ajili ya kuweka mazingira ya utengenezaji wa chakula cha asili kwa ajili ya samaki.

Ufugaji wa Vifaranga vya Samaki

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki mara nyingi huwa ni mgumu. Hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato Changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo ina hali nzuri.

Vifaranga wataweza kuwa samaki wenye uzito wa kutosha katika kipindi cha miezi sita (6). Hii inamaa kuwa katika kipindi hicho awe angalau na uzito wa gramu 500 au zaidi.

Ukuaji wa haraka wa samaki wako na kuwa na uzito unaotakiwa, hutokana na ulishaji wa vifaranga.

Chakula kinategemena na uzito wao, kwa mfano samaki hula 5% ya mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.

Hapa tunazungumzia ulishaji wa chakula cha ziada, sababu chakula cha asili amekipata kwenye ile mbolea iliyowekwa kwenye bwawa.

Vifaranga 100 vyenye gramu 10 kila kimoja basi utahitaji gramu 50 kuwalisha.

Katika hali hiyo ya utunzaji mzuri, itakuchukua miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply