Sifa za Jina Bora La Biashara Tanzania

Kuchagua Jina la biashara Tanzania ni hatua muhimu na inabidi utambue sifa za jina la biashara ila watu wengi wamekuwa hawatilii maanani mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchagua jina la biashara.

1. Jina la biashara liendane na huduma unayotoa

Je unafahamu kwamba jina la biashara linatakiwa liakisi huduma au biashara unayoifanya? Ni jambo jema kutumia jina linaloakisi kile unachokifanya.

Kwa mfano jina kama vile “Samelctro” lifaa kwa kampuni ya vifaa vya kielektroniki, “Pamba LTD” lifaa kwa kampuni ya upambaji au mavazi.

Itakuwa ni jambo la kushangaza kutumia “Samelctro” kwenye mavazi au kutumia “Pamba LTD” kwenye vifaa vya kielektroniki.

Ukizingatia hili mapema utaweza kuitambulisha bidhaa au huduma yako vyema kwa kupitia jina la biashara yako.

2. Jina la biashara liwe fupi na linalo eleweka

Uchaguapo jina la la biashara au kampuni yako kaa chini tafuta jina fupi lenye mvuto na linaloeleweka.

Usitumie majina magumu na marefu kama vile “matunda bora ya shamba”, “rextymyshoes” “mauaborasana”, “John Noe na Rose Mewa Beauty Saloon”, n.k. Chagua jina fupi linalovutia ambalo pia ni rahisi kwa watu kulikumbuka.

3. Jina la biashara linalo eleweka mtandaoni

Katika swala hili nimeshuhudia watu wengi wakichukua majina ya biashara au kampuni bila kujali swala la matumizi ya mtandao. Kwa mfano mtu anaweza kusajili kampuni inayoitwa hope, smart, green nk.

Majina haya huwezi kuyatumia kwenye mtandao kwani tayari yameshatumika katika mambo mengi sana hapa hutoweza kupata huduma kama vile anwani ya tovuti au baruapepe inayoendana na jina la kampuni yako.

Hivyo basi tumia huduma kama vile (Whois) kutazama kama unaweza kupata anwani ya matandao inayoendana na jina la kampuni au laa.

Kumbuka haina maana kampuni kuitwa Moja LTD halafu ikawa na tovuti inayoitwa “mbili.com” hapa utapoteza watu, hawataweza kuifikia tovuti yako vyema.

4. Jina la biashara liwe la kipekee

Kama nilivyoeleza katika hoja zilizopita hapo juu ni muhimu kuhakikisha unabuni jina lenye upekee kwa ajili ya biashara yako.

Epuka kutumia majina yanayofanana na majina mengine.

Kumbuka zipo shereia za kimataifa zinazolinda majina ya kibiashara (Brands) za kampuni mbalimbali majina kama vile Microsofti, Thetoyota, Delli na Vodacomu.

Majina haya ya biashara yatakupelekea kuingia kwenye mgogoro wa kisheria na makampuni husika kwani majina haya yanalandana sana na majina ya kampuni zao.

5. Jina la biashara lizingatie mahitaji ya mbeleni

Inawezekana jina la kampuni au biashara linalofaa leo lisifae tena kwa ajili ya biashara yako baadaya ya miaka mitano.

Hivyo ni vyema kuchagua jina ambalo utadumu nalo katika kampuni yako.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo