Biashara Ya Upigaji wa Picha Tanzania

Biashara ya upigaji wa picha ni nzuri na pia Kama una vifaa vya kisasa vya kupiga picha basi unaweza kuanzisha biashara ya kupiga picha. unaweza kupiga picha matukio yaliyozoeleka kama picha za harusi, wahitimu wa chuo pamoja na picha za mikutano.

JINSI YA KUPATA PESA KUPITIA UPIGAJI WA PICHA

  • Kupiga Picha Biashara Ndogo Ndogo

Siku hizi ni muhimu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kutumia mitandao ya kijamii ili kujitangaza na kupata wateja zaidi. Wanawavutiaje wateja? Ni kupitia picha nzuri na hata video ambazo zinahitaji ubunifu na mtu mwenye uwezo na ujuzi.

  • Kufundisha Kupiga Picha

Kila siku kuna watu ambao wanahitaji kujifunza kupiga picha. Hivyo kutokana na ujuzi wako unaweza kutoa huduma ya mafunzo kuhusu upigaji wa picha kwa watu mbalimbali. Kwa kufanya hivyo unafaidika na fedha unakutana na watu wapya na wenye maarifa na uwezo mbalimbali pia unajifunza na kuongeza ufanisi.

  • Kuanzisha Tovuti

Unaweza kuanzisha tovuti kuhusu tasnia ya upigaji picha maeneo ya kupata vifaa vya kisasa vya picha kwa bei nafuu pia unaweza kuweka picha zako na kuzielezea. Kadri watu wanavyoangalia machapisho yako ndio itakavyokuwa rahisi kwako kupata watu wa kutangaza huduma na bidhaa zao katika tovuti yako na kujipatia fedha.

  • Kupiga Picha za Matukio

Kama unapenda kujichanganya na watu na kuhudhuria matukio basi tambua kuwa unaweza kujipatia fedha. Kwa mfano unaweza kwenda katika sehemu za burudani na kupiga picha watu wakiwa wanafurahi kisha kuwaonyesha picha hizo kisha unaweza kuwa na bei tofauti kulingana na jinsi wahusika wanataka kuzipata picha hizo.

  • Kuhariri Picha

Wapiga picha mashuhuri wanaweza kuwa na majukumu mengi na hivyo kukosa muda wa kufanya kila kazi kwa umakini zaidi. Kama una ubunifu na ujuzi wa kutosha katika upande wa ku edit picha basi unaweza kufanya mawasiliano na wapiga picha ambao tayari wamefanikiwa na kuwaonyesha ujuzi wako wa kuhariri picha kupitia kazi ambazo umeshafanya kisha kufanya makubaliano na kupata fedha.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general