Kilimo Cha Minazi Tanzania

Kilimo cha Minazi Tanzania ni kilimo kizuri sana na ili kupata mnazi ulio bora mkulima ni lazima awe muangalifu wakati wa kupanda minazi.

Mche uliopandwa vibaya huchelewa kukua na hata wakati mwingine hufa pia Mazingira kama vile aina ya udongo, kiasi cha mvua, joto, na mwinuko lazima yaangaliwe kwa makini kabla ya kupanda.

Mazingira Yanayofaa Kulima Minazi

Sehemu zinazofaa kulima zao la minazi lazima ziwe na mvua ya kutosha au ziwe na mabonde yenye unyevu ardhini.

Kwa kifupi mvua isipungue milimita 1000 hadi 2000 kwa mwaka na kiangazi kisichozidi miezi mitatu.

Sehemu hiyo vilevile iwe na joto la kutosha (23 hadi 30 nyuzi joto) na mwinuko kutoka usawa wa bahari usiozidi mita 600.

Minazi inapendelea mwangaza wajua, kwa hivyo isipandwe chini ya miti kama vile miembe au mikorosho.

Uchaguzi Wa Ardhi Ya Kulima Minazi

Ni vyema kufanya uchaguzi wa ardhLinayofaa kwa minazi kabla ya kupanda.

Ardhi Mbaya kwa Kupanda Minazi

Haifai kupanda minazi kwenye ardhi yenye mawe, miamba, jasi na maji yaliyotuama pia Sehemu hizi hazifai kwa sababu mizizi ya minazi inapokutana na moja ya hivi, husababisha minazi kudumaa, kubadilika rangi ya makuti kuwa njano badala ya kijani, huacha kuzaa na hatimaye hufa.

Vile vile ardhi yenye kutuanusha maji zaidi ya siku mbili haifai, kwani husababisha mizizi ya minazi kuoza, hivyo kushindwa kupata chakula na mara nyingi niinazi kufa.

Ardhi Nzuri kwa Kupanda Minazi

Minazi inaweza kustawi katika aina nyingi za udongo, lakini hupendelea zaidi kichanga, tifutifu au kinongo.

Katika seheinu zinazoathiriwa na ukame minazi inaweza kupandwa kwenye maeneo ambayo kina cha maji ardhini wakati wa kiangazi hakizidi mita 3.5 kutoka usawa wa ardhi.

Jinsi Ya Kutayarisha Shamba La Minazi

Baada ya kuchagua sehemu ambayo minazi itapandwa mkulima ni lazima atayarishe shamba mapema kabla ya mvua kuanza. Matayarisho hayo ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kuondoa takataka.

Kufanya hivi hurahisisha kazi za badaaye hasa upirnaji, palizi na kuzuia wadudu kama vile chonga.

Jinsi Ya Kupima Shamba La Minazi

Upimaji wa shamba ni muhimu kabla ya kupanda miche ya minazi na mkulima anaweza kupima shamba lake kwa kuzingatia mambo yafuatayo:

Iwapo mkulima anataka kuchanganya mazao mengine kwenye shamba la minazi kama vile michungwa, minanasi, mipera na migomba, inashauriwa kutumia mita 9 kati ya mnazi na mnazi na Mstari hadi mstari mita 15.

Iwapo mknlima atapendelea kupanda minazi peke yake shambani inabidi atumie nafasi ya mita 9x9x9 pembe tatu.

Nafasi ya aina hii inafaa kwenye sehemu zenye mvua ya kutosha kama Zanzibar, Tanga, Pangani, bonde la Ng’apa na Mikindani.

Sehemu zenye mvua chache kama vile Mtwara, Lindi, Kisarawe, Kibaha na Morogoro inashauriwa kutumia nafasi ya mita 10 kutoka mnazi hadi mnazi na mita 10, kati ya mstari na mstari.

Miche Bora Kwa Kilimo Cha Minazi

Kabla ya mkulima kupanda miche ya minazi hana budi kuchagua miche iliyo bora. Uwe haukushanibuliwa na wadndu au magonjwa.

Uwewenyeafyanamajani yakeyawe kijani. Uwe wenye majani yapatayo sita na uwe nmekaa kitaluni kwa miezi 9.

Uchimbaji wa Mashimo Ya Kupandia Minazi

Ni vizuri mashimo yachimbwe kabla ya mvua’. Kipimo cha kila shimo ni sentimita 60 kwa urefu, upana na kina.

Shimo linapochimbwa udongo wajuu utengwe mbali na udongo wa chini. Baadae changanya udongo wa juu na debe moja la samadi au mboji (compost) kama inapatikana.

Weka udongo wajuu wenye rutuba zaidi kwanza kwenye shimo, halafu panda mche wako katika shimo na rudishia udongo wa chini na kuhakikisha kuwa mche wako umeshindiliwa ili usimame barabara.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

3 Comments
  1. Siku za mbeleni nawaza kununua shamba la minazi hekari moja ili na mimi nianzishe kilimo cha minazi.

  2. Naomba ushauri ardhi yangu ni mfinyazi iko bombeni na nilikua napenda zao la minazi.

Leave a reply