Owner of Wauzaji

Najua Unatamani Kufahamu Mimi ni nani na Pia nina Ujuzi gani Kichwani. Mimi Nimezaliwa Dar Es Salaam na Mpaka Sasa Bado Naishi Kimara Mwisho, Dar E Salaam.

Naitwa Lenald Minja

Napenda sana Kuungana na Wengine ikiwemo Kuwa na Urafiki na Watu Ambao Wanafanya Ujasiriamali wa Mtandaoni Kama mimi.

Mtandaoni Kunahitaji Uvumilivu sana Kwasababu Mpaka leo Nimesha fanyaga Project nyingi sana za mtandaoni na nimepitia changamoto nyingi sana.

Mfano hata Hii website ya Wauzaji.com nimeshawahi kufanya uzembe ikadukuliwa na kisha Nika Jifunza na Kisha nikaanza upya.

Mimi Binafsi Nina Utaalamu wa Search Engine Optimization (SEO) Pia nina Utaalamu wa Hardware Na Software Troubleshooting Pamoja na Motor Vehicle Mechanics.

ELIMU YANGU YA DARASANI
  1. Motor Vehicle Mechanics
  2. information Technology
ELIMU YANGU BINAFSI
  1. Search Engine Optimization (SEO)
  2. Computer User Support
  3. Hardware Troubleshooting
  4. Software Troubleshooting
  5. interpersonal Relationship

VITU NINAVYO VIPENDA

1. Napenda Kuwasaidia Watu

Kutokana na Kusoma na Kupenda sana Maswala Ya Teknolojia nimekuwa najikuta napenda sana Kuwasaidia watu kwenye mambo yanayohusiana na Teknolojia ikiwemo utumiaji wa vifaa vyao vya mawasiliano.

2. Napenda Kufanya Mazoezi

Kutokana na Kutambua Ya kuwa Afya Njema inachangia sana utendaji mzuri wa kazi hivyo nimejikuta Napenda sana Kufanya Mazoezi ili kulinda Afya yangu kwa Ujumla.

3. Napenda Kusikiliza Muziki

Binafsi Napenda sana Kusikiliza Muziki Kwa Sababu muziki umekuwa unaniburudisha sana Endapo nikiwa Nimechoka Kimwili au Kiakili.

VITU NISIVYO VIPENDA

1. Sipendi Mwenzangu Ashindwe

Najisikiaga sana Vibaya Endapo nikiona mtu anapata changamoto katika utumiaji wa vifaa vya Teknolojia Kwasababu mimi ninao uwezo wa kuvitumia na Kumuelekeza Tena kwa ufasaha.

2. Sipendi Kuikwepa Teknolojia

Kutokana na Teknolojia kurahisisha kazi sipendi kuona mahala ninapofanya kazi wanakuwa nyuma kwenye utumiaji wa vifaa vya Teknolojia kutokana na kuto kuweza kuviendesha kwa Ufasaha.

3. Sipendi Kusifiwa Kwenye Kazi

Kufanya Kazi Kwa Juhudi na Maarifa nikiwepo kazini ni wajibu wangu hivyo basi sipendagi kuona mtu ananisifia kwasababu ni moja ya wajibu wangu Nikiwepo Eneo La Kazi.

Mawasiliano Yangu

Nakuahidi kama ukinitumia email basi mimi Nitaijibu ndani ya Dakika 59 kwasababu napenda kujali muda wa wenzangu.

Email Yangu Binafsi [email protected]

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general