Tangaza na Sisi

Kama unawaza biashara yako inawafikia walengwa wako wote wa mtandaoni basi nakuomba uwaze tena kwa undani zaidi.

Karibu sana Wauzaji.com hapa utapata taarifa za jinsi ya kuungana na Sisi.

Utangulizi wa Wauzaji

Mimi naitwa Lenald Minja mimi ndio nipo nyuma ya Wauzaji. Acha Nikuambie historia pamoja na mwongozo wa matangazo kwa ajili ya Biashara yako.

Wauzaji nilianza Kuiwaza nikiwa darasani mwaka 2019 na nikaanza kuitengeneza rasmi mwaka 2020 na nikaiweka online mwaka 2021 nikifanya kama hobby.

Lakini baada ya mwaka 1 ikawa website maarufu sana Tanzania ambapo wateja wanakuja kuwangalia Wauzaji waaminifu wa Tanzania.

Mambo Yaliyomo Ndani Ya Wauzaji

Website Hii ya Wauzaji ndani yake inahusiana na mambo mbalimbali ila Kwa Ujumla asilimia 99 ya website Hii inahusiana na Mambo yafuatayo;

 • Orodha ya wauzaji
 • Review za wauzaji
 • Maelezo ya biashara
 • Maelezo ya ufugaji
 • Maelezo ya kilimo
 • Maelezo ya maisha
 • Na vitu vingine vinavyofanana na hivi.

idadi ya Watembeleaji

 • Daily visits: 3,000+
 • Daily pageviews: 4,500+
 • Monthly pageviews: 120,000+ (85% Organics)
 • Email list: 2,500+

Tuna update hizi taarifa kila baada ya miezi 3 ili ziendane na uhalisia wa kupanda na kushuka kwa idadi ya watembeleaji.

Fursa za Kutangaza Kwetu

Tunatambua uwepo wa watu wanaohitaji kujitangaza kwetu na sisi pia tunawalenga wale ambao wana malengo ya kufika mbali na tayari Kuna Baadhi Tumeshaungana nao wakiwemo Bluehost, Namecheap pamoja na wengine.

Aina za Matangazo Tunayopokea

Tunazo option 2 za matangazo ambazo zitakuwezesha kuungana na sisi katika hii website yetu ya wauzaji.

1. Tangazo La Reviews

Matangazo ya reviews yanahusisha kuandika post ya kuwa wewe ni muuzaji wa bidhaa flani na matumizi ya bidhaa yako, Na mawasiliano yako pamoja na kukuweka pia kwenye post zinazofanana kwa ukaribu na bidhaa yako.

2. Tangazo La Bango

Matangazo ya bango yanategemea na saizi ya bango pamoja na sehemu ambapo tangazo lako litawekwa.

 • 468*60 Sehemu ya juu ya website
 • 468*60 Sehemu ya kati baada ya post
 • 300*250 Sehemu ya pembeni ya website
Bei Ya Matangazo

Kama unataka kupost tangazo au kuungana na mimi karibu sana tuzungumze.

Mawasiliano Yangu

Nakuahidi kama ukinitumia email basi mimi Nitaijibu ndani ya Dakika 59 kwasababu napenda kujali muda wa wenzangu.

Email Yangu Binafsi [email protected]

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general