Utangulizi wa Kilimo Bora Cha Parachichi Tanzania

Kilimo cha parachichi kinaendelea kukua sana Tanzania Pia kilimo hichi cha maparachichi hakihitaji fedha nyingi na bali ni subira ya ukuaji wa matunda ya Parachichi.

Tanzania kilimo hichi kimeanza kushika kasi zaidi mwaka 2015 ambapo baadhi ya watu walijitokeza na kuelezea mafanikio waliyopata kutokana na kilimo cha parachichi.

Nchi za Ulaya kama Denmark, Ufaransa, Uingereza, Norway na Uholanzi zimeonyesha kufurahishwa na kilimo cha maparachichi yanayotoka nchi za Afrika Mashariki hususani Tanzania.

Mikoa inayolima Parachichi Kwa Wingi

Mikoa ya tanzania iliyojikita zaidi na uzalishaji wa kilimo cha zao la maparachichi ni Kilimanjaro, Mbeya, Njombe na Iringa. Hii ni kutokana na hali ya hewa ya baridi iliyopo katika mikoa hiyo.

Wakulima wengi wanaojihusisha na kilimo cha parachichi huuza katika soko la nje. Wengi wao wanalima zaidi aina ya parachichi inayoitwa Hass, kwa sababu parachichi hii ina sifa kubwa ya kukaa muda mrefu bila kuoza. Parachichi la aina hii hutambulika kwa muonekano wa ngozi yake ambayo huwa inakuwa na vipele.

Baadhi ya makampuni ambayo yamewanufaisha wakulima wadogo wa zao hili la parachichi kwa kununua matunda hayo na kuyasafirisha nje ya nchi ni kampuni ya Africado iliyopo Kilimanjaro ambapo watu zaidi ya 2,000 wamenufaika na zao hilo kupitia kampuni hiyo.

Licha ya kuuza zao hilo, watu waliopo karibu na kampuni ya Africado wamenufaika na ajira. Kampuni nyingine zinayofahamika kwa usafirishaji wa zao hili la parachichi nje ya nchi ni kampuni ya Rungwe Avocado Limited na Cuser Africa Limited ambazo zote kwa kiasi kikubwa zimewanufaisha watanzania wanaojihusisha na kilimo cha parachichi.

Ni muhimu kwa mkulima yoyote anayetaka kuanzisha kilimo cha parachichi kuwa makini, kwa sababu baadhi ya wazalishaji wa miche ya maparachichi wamekuwa sio waaminifu hivyo unaweza kununua miche mingi na kupata hasara.

Inashauriwa kuwasiliana na wataalamu wanaohusika na kilimo cha maparachichi ili kutengeneza mpango mzuri wa uzalishaji na mwisho wa siku kupata faida.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

3 Comments
  1. Nimefurahishwa na Mtandao wenu ila mimi napenda sana Kuanza kilimo cha parachichi na ipo siku Nitaanza.

  2. Natafuta soko la kuuza parachichi zangu, Tafadhali sana naomba msaada wenu kupata mtandao wa wanunuzi wa parachichi aina ya hass.

Leave a reply