Utangulizi wa Kilimo Bora Cha Mihogo Tanzania

Kilimo cha Mihogo Tanzania ni moja ya kilimo ambacho kinalimwa sana tanzania hasa kutokana na tabia yake ya kuvumilia sana hali ya ukame.

Tanzania wakulima wengi hasa wadogo hupendelea kuchanganya zao la mihogo pamoja na mazao mengine kama maharage, kunde, mbaazi, njugu mawe n.k.

Mambo ya kuzingatia katika kilimo cha mihogo.

1. Kilimo cha Mihogo kinaweza kuchukua hadi miezi 18 kuwa tayari kwa ajili ya mavuno, ambapo inahitaji miezi 8 ya kuendelea kukua katika hali yenye joto na hufanya vizuri zaidi ikikua kwenye jua.

2. Mihogo inaweza kuvumilia hali ya ukame na kuweza kukua kwenye udongo usio na rutuba. Kawaida sio rahisi kwa muhogo kushambuliwa na wadudu na magonjwa ya mimea.

3. Mihogo inaweza kuhifadhiwa chini ya ardhi kwa miaka miwili bila kuoza.

4. Mihogo inajulikana kwa majina mengi ikiwa ni pamoja na yucca, manioc, mandioca, mizizi ya yucca, casaba, na tapioca.

5. Watu wengi hupendelea kula mihogo kwa sababu ni rafiki kwa afya na chakula kwa ujumla.

6. Muhogo hutengenezwa katika njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemsha, kuoka, kukaanga, kuchoma, na kwa Tanzania watu hutengeneza unga wa muhogo na kupika ugali wa muhogo.

7. Kuna aina mbili za muhogo ambazo ni muhogo mtamu na mchungu. Muhogo mchungu hutumika kwenye mikate na keki.

8. Mihogo ina kalori nyingi pamoja na wanga.

9. Shirika la Kansa huko Marekani linawaonya watu wenye aleji na mipira ya Latex kuwa makini na mihogo kwani wanaweza kupata aleji ikiwa watatumia mihogo.

10. Inashauriwa kutokula mihogo ikiwa mibichi kwa sababu ndani yake kuna kitu kinaitwa cyanide ambacho si nzuri kwa afya ya binadamu na kinaweza kupelekea binadamu kupata matatizo ya kutembea, magonjwa ya chronic pancreatitis.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo