Utangulizi wa Kilimo Cha Bamia

Kilimo cha Bamia kwa Tanzania ni kilimo maarufu sana kwasababu bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto na zao la bamia hutumika kama mboga.

Matumizi Ya Bamia

Bamia hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine.

Jinsi Ya Kupanda Bamia

Mbegu mbili za bamia zipandwe kwenye shimo moja na nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari.

Kwa zile aina zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.

Jinsi Ya Kupalilia Bamia

Hakikisha shamba la bamia ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza.

Jinsi Ya Kumwagilia Bamia

Kwenye shamba la bamia iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini.

Wadudu Wanaoharibu Zao La Bamia

Wapo wadudu wanaoshambulia zao la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na utitiri mwekundu.

Magonjwa Ya Zao La Bamia

Magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri sana zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo.

Mambo Ya Kuzingatia Kwenye Kilimo

  • Tumia mbegu bora ya bamia
  • Panda bamia kwa nafasi
  • Mwagilia maji ya kutosha kwenye bamia
  • Palilia shamba vizuri
  • Vuna bamia zako kwa wakati unaotakiwa

Jinsi Ya Kuvuna Bamia

  • Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
  • Kiasi cha kilo 8000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
  • Hakikisha unavuna bamia na kikonyo chake, kisu kinaweza kutumika kwa kuvuna
Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply