Utangulizi wa Kilimo Bora Cha Alizeti Tanzania

Kilimo cha alizeti Tanzania kimechangia kwa kiasi kikubwa kuwainua wakulima kiuchumi na kuongeza pato la taifa Pia Mbegu za zao la alizeti hutengeneza mafuta ambayo yanatumika kupikia.

Makapi yanayotokana na mbegu za alizeti ni chakula bora kwa mifugo. Kwa mujibu wa takwimu kutoka  kitengo cha mbegu za mafuta katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mbeya, mkulima anaweza kuvuna hadi magunia matano ya alizeti katika hekta moja ya shamba la alizeti.

Kilimo cha Alizeti hulimwa kwa wingi mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Rukwa pamoja na Manyara.

Kilimo cha Alizeti hutegemea sana hali ya hewa ya eneo husika.

Maeneo yenye mvua nyingi zao la alizeti hupandwa mwishoni mwa Januari hadi katikati ya Februari, wakati katika maeneo yenye mvua kidogo mkulima anaweza kupanda kuanzia mwezi Desemba hadi katikati ya mwezi wa kwanza.

Adui mkubwa wa kilimo cha alizeti ni ndege ambao huweza kuteketeza hadi asilimia 50 ya mazao yote shambani, mara nyingi inashauriwa kutopanda zao la alizeti karibu na msitu au pori kwasababu ya uwepo wa ndege.

Mkulima anayefanya au anayetarajia kufanya kilimo cha alizeti anapaswa kuwa na mbinu mbadala ya kuepuka mashambulizi ya ndege. Wengi hutumia sanamu, makopo au hukaa na kufukuza makundi ya ndege wenyewe.

Bila ya kuweka ulinzi shambani kwako, ndege wanaweza kuharibu mazao yako yote. Mbali na ndege, aina hii ya kilimo pia huweza kushambuliwa na magonjwa mengine kama vile madoa ya majani, kuoza kwa mizizi na hata virusi.

Ili kuepukana na magonjwa ya aina hiyo, ni vizuri kufanya kilimo cha alizeti cha mzunguko wa mazao na kupanda mbegu safi ambazo zimethibitishwa na wataalamu, kuchoma masalia kila baada ya msimu kumalizika na kutumiwa dawa kuua wadudu endapo mazao yako yataonyesha dalili ya kudhoofika.

Ni muhimu kutafuta wataalamu wa masuala ya kilimo cha alizeti pale unapohitaji msaada.

Alizeti ni zao zuri sana la biashara na wakulima wengi zaidi wamekuwa wakijitika katika aina hii ya kilimo. Japokuwa uwekezaji katika kilimo hiki cha alizeti umekuwa mdogo tofauti na mazao mengine japo kilimo hiki kimeonyesha mafanikio makubwa hapa nchini.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

2 Comments
  1. Nimefurahi sana kwa utangulizi huu wa kilimo cha Alizeti.

Leave a reply

Wauzaji
Logo