Biashara Ya Ufugaji wa Nguruwe na Mambo Ya Kuzingatia

Gharama za Ufugaji wa nguruwe faida zake pamoja na changamoto na mbinu zilizopo katika ufugaji bora wa nguruwe kisasa na kibiashara Tanzania

1. Chagua koo ZA nguruwe zinazozalisha vyema
  • Uchaguzi wa koo huchangia zaidi ya asilimia 80 katika mafanikio ya ufugaji wa nguruwe, chagua koo amabayo ina  zalisha watoto wengi na wenye afya.
  • Kwa mfugaji wa nguruwe ambaye anatarajia kununua nguruwe kutoka kwa mfugaji mwingine, Zingatia sana kumbukumbu zilizo wekwa na mfugaji yule na cha msingi ziwe sahihi hii itakupa picha ya kujua uzazi wa nguruwe huyo.
2. Jenga banda bora la ufugaji WA nguruwe
  • Jenga banda la Nguruwe ambalo linaendana na idadi na ukubwa wa nguruwe, banda ambalo halitapitisha mwanga mkali wa jua, upepo mkali.
  • Pia litakalo himili mikiki mikiki ya nguruwe wakorofi, hii itasaidia kupunguza usumbufu na bugudha kwa nguruwe na watazaliana bila shida.

Kwa nguruwe anayeishi katika nyumba yenye bugudha na usumbufu uzalishaji wake upungua sana uzalushaji.

3. Zingatia afya bora katika ufugaji WA nguruwe
  • Sote tunafahamu afya ni kitu cha msingi sana iwe kwa binadamu na hata mnyama pia, Hivyo Afya bora ya nguruwe ni kitu cha msingi sana kuzingatiwa kwa kwa nguruwe asiye na afya bora udhoofika na uzalishaji wake hushuka kwa kiwango kikubwa sana.

Afya bora hutokana na kumpa Chanjo dhidi ya magonjwa kama minyoo.

4. Walishe nguruwe chakula bora
  • Chakula cha nguruwe ni muhimu kiandaliwe kulingana na umri wa nguruwe na mahitaji katika mwili wa nguruwe.
  • Chakula cha nguruwe kiwe katika uwiano sahihi hii, chakula ambacho kita kidhi mahitaji ya mwili na uzakushaji kuwa mkubwa.
  • Nguruwe apatiwe chakula chenye vyanzo vya madini, vitamin na protini.
  • Vyakula venye vyanzo vya protini husaidia sana katika kujenga mwili.
  • vyakula vya Vitamin na madini ni vyakula venye vinavyohitajika kwa wingi hasa calcium na phosphorus kwa nguruwe wa kunenepesha na walioachishwa kunnyonya.
  • Epuka kuwapa nguruwe chakula chenye chumvi nyingi kwani hii itamfanya nguruwe kunywa maji mengi sana na matokeo yake nguruwe huarisha sana natimaye ukuaji wake huwa wa polepole.

Hata hivyo kumbuka chumvi uongeza radha ya chakula na uwekaji wake katika mchanganyo wa chakula uwe ni asilimia 0.5 tu

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

2 Comments
  1. Asante Kwa Elimu hii napenda sana siku moja niwe nafanya Biashara ya ufugaji wa Nguruwe.

Leave a reply