Ufugaji wa Mbuzi na Kondoo Tanzania

Mbuzi na kondoo ni wanyama ambao ufugaji wao wa Tanzania ni wa gharama nafuu pia ni wavumilivu wa ukame na maradhi tofauti na mifugo mingine.

Mbuzi na Kondoo wana umbile dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na nguvu kazi ndogo na hata kwa wenye kipato kidogo.

Kuzaa kwao kwa muda mfupi kuna mwezesha mfugaji wa mbuzi na kondoo kuwa na mifugo mingi kwa muda mfupi.

Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi, sufi na mazao mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.

Jinsi Ya Kufuga Kondoo na Mbuzi

 1. Kondoo na Mbuzi wafugwe kwenye banda bora.
 2. Walishwe chakula sahihi kulingana na umri.
 3. Kuzingtia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa.
 4. Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.
 5. Kuzalisha nyama, maziwa, sufi bora unaokidhi mahitaji ya soko.

Banda zuri La Ufugaji wa Mbuzi na Kondoo

 1. Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali (hatari) na wezi.
 2. Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.
 3. Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.
 4. Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.

Ujenzi wa Banda La Kondoo na Mbuzi

 • Banda lijengwe kwa kutumia vifaa vilivyopo eneo husika na kwa kuzingatia uwezo wa mfugaji.
 • Kuta ziwe imara na zinazo ruhusu mwanga na hewa ya kutosha.
 • Mlango uwe na ukubwa wa 60X150 sentimeta.
 • Sakafu iwe ya udongo / zege ya kichanja unaweza kutumia mabanzi / mianzi na iruhusu kinyesi na mikojo kudondoka chini.
 • Chumba cha majike na vitoto kiwe na sentimeta 1.25 kati ya fito na fito au papi na papi, chumba cha mbuzi na kondoo wakubwa kiwe na sentimeta 1.9 kati ya mbao na mbao.

Jinsi Ya Kuchagua Kondoo na Mbuzi wa Kufuga

Lengo ni kuboresha uzalishaji na kupata kizazi bora kuna aina nyingi za mbuzi na kondoo wa kufugwa kulingana na mazingira na mahitaji ya mfugaji.

Uchaguzi unaweza kufanyika kuangalia umbile, uzalishaji na kumbukumbu za wazazi kama vile umbo kubwa, ukuaji wa haraka uwezo wa kutunza vitoto na kutoa maziwa mengi.

Mbuzi Wazuri Kwa Maziwa

 1. Saanen,
 2. Norwegian na
 3. Toggenburg na chotara wao

Kondoo Wazuri Kwa Nyama

 1. Black head Persian (bhp)
 2. Masai red
 3. Suffolk na
 4. Hampshire.

Kondoo Wazuri kwa Sufu

 1. Merino
 2. Lincoln

Kondoo Wazuri kwa Nyama na Sufu

 1. Corriedale
 2. Romney

Nchini kwetu kondoo wanaopatikana kwa wingi ni black head Persian, masai red dopper

Sifa za Mbuzi na Kondoo Jike

 1. Historia ya kukua upesi
 2. Kuzaa mapacha
 3. Kutunza watoto

Sifa za Mbuzi na Kondoo Dume

 1. Miguu iliyo nyooka na yenye nguvu
 2. Mwenye kokwa mbili zilizo kaa vizuri a kunyooka
 3. Mwenye uwezo na nguvu za kupanda
 4. Asiwe na ulemavu

Utunzaji wa Watoto wa Mbuzi na Kondoo

 1. Hakikisha kitoto kinapata maziwa ya mwanzo (dang’a) siku ya kwanza-3.
 2. Kama kinanywesha kipewe lita 0.7-0.9 kwa siku maziwa haya ni bora kwa kuwa yana viinilishe na kinga dhidi ya magonjwa
 3. Kama mama hatoi maziwa au amekufa kondoo au mbuzi mwingine anae nyonyesha anaweza kusaidia kukinyonyesha.
 4. Kitoto kinyonye kwa wiki 12-16 baada ya wiki2 kuzaliwa pamoja na maziwa apewe chakula kingine kama nyasi ili akuze
 5. tumbo lake pia apewe maji ya kutosha.
 6. Aachishwe kunyonya akifikisha miezi 3
 7. Vipewe chanjo ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam

Umri wa Kupandisha Kondoo na Mbuzi

Mbuzi na kondoo wakitunzwa vizuri wanaweza kupandishwa wakiwa na umri wa miezi 8-12 kwa walioboreshwa miezi 18-24 kwa mbuzi wa asili iatategemea na afya alonayo pia inashauriwa apandishwe akiwa na uzito wa kilo 12.

Dalili za Mbuzi na Kondoo Anayetaka Kupandwa

 1. Hutingisha mkia
 2. Hutoa ute mweupe ukeni
 3. Hufuata dume
 4. Hamu ya kula hupungua
 5. Hukojoa mara kwa mara
 6. Uke huvimba na huwa mwekundu kuliko kawaida
 7. Huangaika mara kwa mara na kupiga kelele
 8. Kwa mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa.
 9. Mbuzi na kondoo mwenye dalili hizi apelekwe kwa dume na uchunguze tena dalili za joto baada ya siku 19-21
 10. Msimu mzuri wa kuzaa ni baada ya mvua.

Utunzaji wa Mbuzi na Kondoo Mwenye Mimba

 1. Mbuzi hubeba mimba kwa muda wa miezi 5
 2. Apewe chakula cha ziada 0.2-0.7.
 3. Apewe nyasi,miti malishi na mikunde mchanganyiko kilo 1.8-2.5 kwa siku

Dalili za Mbuzi na Kondoo Kukaribia Kuzaa

 1. Huangaika kwa kulala na kuamka mara kwa mara
 2. Hujitenga na kundi na hufuata sehemu kavu na yenye kivuli
 3. Hutokwa na ute mzito ukeni
 4. Hupiga kelele
 5. Pindi ukiona dalili hizi muandalie sehemu maalum ya kuzalia na muwekee maji ya kutosha.
Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo