Tiba za Ugonjwa wa Ndui kwa Kuku

Ugonjwa wa ndui ni ugonjwa wa kuku ambao unakwamisha ufugaji wa kuku kwa kutumia dawa za asili pia tambua ugonjwa wa ndui ni ugonjwa unaoenezwa kwa virusi.

Dalili za ugonjwa wa ndui

  • Ugonjwa wa ndui utaona kuku wako wamepata mapele kwenye kichwa yenye rangi ya kahawia, mapele hayo yanaweza kuziba mpaka macho na kufanya kuku wako wasione kabisa na kusababisha kuku wako wakashindwa kula hivyo wakadhoofika kabisa na hatimaye kufa.

Ugonjwa huu huwapata kuku wa rika zote lakini huathiri sana vifaranga.

  • Mara nyingi magonjwa ya virusi ni magonjwa ambayo hayana tiba lakini yana kinga. Wachanje kuku wako hasa vifarnga wanapokua wamefikia umri wa siku 56 yani wiki nane(8).

Jinsi ya kutibu ndui kwa kuku

  • Kwanza kabisa nunua OTC 20% pamoja na vitamin, wachanganyie kuku wako kwenye maji ili kuwaepusha na magonjwa nyemelezi kwa sababu wanapokua wanashambuliwa na ugonjwa wa ndui ugonjwa huu una sifa ya kupunguza sana kinga ya mwili.
  • Kinga ya mwili kwa kuku wako inashuka sana hivyo inakua rahihisi kwa kuku wako kuambukizwa magonjwa mengine, kwa hiyo unapokua unawapatia OTC20% pamoja na VITAMIN inawasaidia kuboost kinga ya mwili.
  • Jinsi ya kutibu ugonjwa wa ndui? Kwanza kabisa tafuta mafuta ya ng’ombe yanapatikana masokoni hasa masoko makubwa makubwa unaweza ukanunua maziwa freshi ambayo hayajawekewa maji ukayagandisha alafu ile samli ya juu ukaichukua kama mafuta ya ng’ombe.
  • Unayafanyaje sasa hayo mafuta ya ngo’mbe? Mafuta hayo unawapakaa kuku wako maeneo ambayo yana hayo madonda. Unapaka mara mbili kwa siku asubuhi na jioni ndani ya siku mbili.

Baadae yale madonda kwa kuku yanakua yamelainika na unaweza kuyabandua bila shida yoyote na kuku wako wanakua vizuri na wanakua wamepona.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

6 Comments
  1. Hivi ugonjwa wa ndui kwa kuku hauwezi kushambulia vifaranga chini ya huo umri wa siku 56?

  2. Kuku wangu tayari wameupata ugonjwa wa ndui nafanyaje kutibu huu ugonjwa kwa kuku wangu?

  3. Vip kama vifaranga wa kuku wameshaathirika na ndui hadi baadhi yao macho yamevimba kabisa je kwa kutumia hizo njia za tiba ya ndui ulizozisema wanaweza wakapona kabisa?

Leave a reply

Wauzaji
Logo