Siri za Mafanikio Katika Biashara Tanzania

Siri mbalimbali za mafanikio katika maisha pamoja na mafanikio kwenye biashara ambazo matajiri na watu waliofanikiwa hawazisemagi kwa uwazi.

1. Fedha Siyo Makaratasi

Watu wengi wamekuwa wanafikiria fedha ni yale makaratasi au sarafu ambazo tunazishika Na hapa ndipo wengi wanapokwama, kwa sababu wanakosa ule msingi muhimu kuhusu fedha. Kwa kukosa msingi muhimu kuhusu fedha, watu wanashindwa kuzipata kwa wingi na hata kuzitumia vizuri.

Fedha ni wazo ambalo lina thamani. Fedha ni matokeo ya mtu kuwa na wazo ambalo linaongeza thamani kwa wengine. Bila ya thamani hakuna fedha.

Hivyo kama unataka fedha zaidi, lazima ujue thamani gani unatoa kwa wengine.

2. Kipato Kimoja NI Utumwa

Kuwa na chanzo kimoja cha kipato pekee ni utumwa. Huwezi kuondoka kwenye umasikini kama unategemea kipato chako kitoke sehemu moja pekee.

Kama umeajiriwa pekee, hata kama unalipwa kiasi kikubwa cha fedha, bado unabaki kwenye umasikini, pia Kama unafanya biashara na unategemea wateja wachache nayo pia inakuweka kwenye umasikini.

Utaondoka kwenye umasikini kwa kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Hiyo kama unataka usikaukiwe na fedha, kuwa na vyanzo vingi vya kipato.

3. Matumizi NI Bomu

Watu wengi wamekuwa wanaanza maisha na kipato kidogo, na yanaenda. Kipato kinaongezeka na matumizi yanaongezeka, kila kipato kinapoongezeka na matumizi pia yanaongezeka.

Matumizi ni bomu kama hayatadhibitiwa. Matumizi yana tabia ya kuongezeka pale tu kipato kinapoongezeka.

Huwezi kuondoka kwenye umasikini kama huwezi kuyadhibiti matumizi yako. Haijalishi unatengeneza kipato kikubwa kiasi gani, matumizi ni bomu, usipolitegua litakulipua.

4. Madeni NI Utumwa

Kuna madeni mazuri na mabaya, na masikini wote huwa wapo kwenye madeni mabaya. Madeni mabaya ndiyo yanawafanya watu kuwa watumwa, wanajikuta wanafanya kazi sana kulipa madeni, halafu wanakopa tena.

5. Biashara NI Mkombozi

Kwa zama tunazoishi sasa, mkombozi pekee, kitu pekee kitakachokuwezesha kuwa na maisha mazuri ni kuwa na biashara yako. Hivyo ni muhimu sana uwe na biashara kama unataka kutoka kwenye umasikini.

6. Uwekezaji NI Kijakazi Wako

Kwenye kuondokana na umasikini na kufikia uhuru wa kifedha, ni lazima fedha ziwe zinakufanyia kazi wewe na hapa ndipo unapohitaji kuwa na uwekezaji, ambao unafanya kazi ya kuuzalishia fedha, hata kama wewe umelala.

7. Kodi NI Uwekezaji

Kodi ni gharama unayolipa kwa kuishi kwenye jamii iliyostaarabika. Kodi tunazolipa ndiyo zinazoleta huduma mbalimbali tunazozitegemea kwenye jamii.

Huduma za afya, huduma za elimu, ulinzi na usalama, miundombinu kama barabara na mengineyo ni matokeo ya kodi tunazolipa.

Hivyo kodi ni uwekezaji ambao kila mmoja wetu anapaswa kuufanya ili tuwe na jamii bora na Tunapaswa kuondokana na dhana potofu kwamba kodi ni kitu kibaya.

8. Bima NI Mkombozi

Kuna hatari mbalimbali ambazo zinatuzunguka kwenye maisha, na kadiri unavyopiga hatua kifedha, ndivyo hatari zinakuwa kubwa zaidi.

Bima huwa unachangia kiasi kidogo cha fedha, lakini unapopata tatizo, unalipwa kiasi kamili cha fedha au mali ulizopoteza.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply