Sababu zinazozuia Mafanikio Katika Biashara

Jinsi Ya Kufanikiwa Katika Biashara Kwa Tanzania Kuna endana Sana na Tabia Ulizonazo Hivyo Hizi ni Baadhi Ya Siri za Kufanikiwa Katika Biashara

Sababu za Kutokufanikiwa Katika Biashara

Kukosa maarifa ya kutosha ya fedha

Unajua fedha inahitaji maarifa fulani kwenye namna ya kuingiza, kuwekeza pamoja na kusimamia fedha Sasa watu wengi hawana hii financial literacy au financial knowledge.

Aina ya marafiki

Kuna aina ya marafiki kama ukiwa nao wanaweza wakakupelekea kujikuta nawe ukipoteza hela zako. Haswa wale wasio na nidhamu ya fedha ambao ni wapenda kufanya anasa na matumizi yasiyo na mpangilio.

Tabia baadhi zisizo rafiki

Pia kuna tabiaa mbazo kama mtu atakuwa nazo basi ni rahisi sana kwake yeye kujikuta akipoteza pesa zake. Miongoni mwa tabia hizo zimeongelewa hapa chini.

Tabia zinazofanya watu wasifikie Mafanikio

Kutokuwana bajeti

Bajeti ni kama vile ramani kwa mtu ambayo humuongoza kuhusu kufaya matumizi yake. Ni tabia ya kuwa na bajeti ndiyo inamsaidia mtu kufanya matumizi yake kwa kimahesabu na kuepuka matumizi mabovu ya pesa.

Kuendekeza Tamaa

Pesa haiongozwi kwa matamanio (tamaa) lasivyo itaishia kuteketea na kupotea kwa upesi sana. Pesa inabidi iongozwekwa fikra. Yaani iwe inatumiwa kwa mipango na kufikiria kwa umakini sana ili kuepuka matumizi ya tamaa.

Kufuata mkumbo

Tabia ya kuiga wengine na kufanya matumizi ya kufuata mkumbo pia inapelekea watu wengi kupoteza hela zao. kwa sababu hujikuta wanajishindanisha na wengine na kujiingiza kwenye matumizi makubwa mno yasiyo hata na ulazima.

Kupenda sana starehe

Starehe ni gharama Kama ukiwa ni mtu wa kuendekeza starehe basi fedha zako zipo hatarini sana kupotea kwenye matumizi ya gharama za kumudu starehe hizo.

Kuna baadhi ya starehe sio za lazima sana ambapo kama mtu usipojizoesha sana kupenda starehe unaweza kujikuta ukiokoa pesa zako nyingi sana kutopotea.

Kutokuweka kuweka akiba

Akiba ni muhimu sana katika kuokoa pesa zako Hivyo kama haufanyi saving kuna uwezekano mkubwa wa kuishia kupoteza hela zako za ziada.

Uoga wa kupata hasara

Tabia ya kuwa na uoga inaweza kumpelekea mtu kutofanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi ya pesa zake sababu ya uoga wa kufilisika mtu anaacha kuwekeza pesa yake na kuishia kuifanyia matumizi ya starehe nyingine.

Tabia ya kuahirisha mambo

Inaweza ikatokea fursa kubwa ya uwekezaji au inayohitaji mtu kuwekeza pesa zake ili kupata pesa nyingi zaidi.

Lakini unakuta mtu anajipanga kuitumia hela yake namna hiyo kisha kuahirisha kufanya hivyo na kujikuta kapoteza nafasi au fursa ya kupata pesa nyingi zaidi.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

2 Comments
  1. Napendaga sana makala zenu kuhusu biashara ni nzuri sana.

Leave a reply

Wauzaji
Logo