Sababu na Dawa Ya Kuzuia Kuku Kula Mayai Yake

Sababu za kuku kula mayai yake

Sababu za kuku kula mayai yao ni nyingi na ndio maana nimekuandikia ili uweze kuzitambua sababu hizo pamoja na jinsi ya kuzuia kuku kula mayai yao wenyewe

 • Tabia yao tu

Hii ni sababu ya kuku kula mayai Hapa utakuta ndo uzao wao wanatabia ya kula mayai hivyo kuku hufanya muendelezo wa kula mayai

 • Kuto kupata chakula cha kutosha

Hii ni moja ya sababu za kuku kula mayai kwakuwa kuku akikosa chakula inapelekea kuleta sababu ya kuku kula mayai

 • Kukosa madini joto

Hii inaweza kuwa ndo sababu ya kuku kula mayai endapo kuku wakikosa madini joto ni lazima wale mayai na hata kulana wao wenyewe, na jua kwamba kwenye yai kuku huwa anatafuta lile ganda la juu pekee sema anapo donoa na kulipasua yai hujukuta anakula na ute na kiini ila yeye lengo lake hasa ni ganda la juu

 • Mayai kukaa muda mrefu bila kukusanywa baada ya kutaga

Hii ni sababu za kuku kula mayai kwasababu mayai yanapo kaa muda bila kukusanywa na kama yapo sehemu ya wazi sana hupelekea kuku waanze kutest na kushangaa nini hiki cheupe? katika kushangaa ni kitu gani hiki cheupe cha mviringo hujikuta wanatest kudonoa na matokea yake ni kupasua yai na kupelekea sababu za kuku kula mayai.

 • Kuku kutagia sehemu nyeupe sana yenye mwanga mkari hupelekea kuku kula mayai.
 • Lishe mbaya
 • Nafasi ndogo
 • Vyombo havitoshi
 • Kukosa shughuli
 • Banda chafu (Manyoya)
 • Ukoo

Jinsi ya kuzuia kuku kula mayai yake

 • Chakula cha kutosha ni muhimu sana, ili kuwafanya wasitake kula mayai ili kushiba
 • Mayai yakusanywe mara tu anapo taga na usiyaache muda mrefu bandani
 • Sehemu ya kutagia iwe na giza la kutosha ili kufanya kuku ashindwe kuona yai alilo taga
 • Madini joto ni muhimu sana
 • Kuku wenye tabia za kula mayai unaweza chinja au kuuza
 • Kuweka idadi ya kuku inayolingana na sehemu ulionayo
 • Usizidishe mwanga
 • Banda liwe safi
 • Weka vyombo vya kutosha
 • Wape lishe bora
 • Kata midomo ya juu
 • Epuka ukoo wenye tabia hizo
Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

5 Comments
 1. Leo Ndio Nimefahamu Kwanini kuku wangu wanakulaga mayai yao.

 2. Njia ya kukata mdomo wa kuku nafikili ni njia iliyo sahihi na salama ya kuzuia kuku kula mayai.

Leave a reply