Njia za Jinsi Ya Kutangaza Biashara Tanzania

Kutangaza Biashara ni muhimu Ili uweze kupata kupata wateja kwa wingi zaidi na ili ijulikane kwa wateja wengi zaidi hivyo basi matangazo yanasaidia sana katika kukuza biashara yako kwa ujumla.

Faida za Kutangaza Biashara

Kuongeza Wateja

Kadri unavyofanya matangazo ya biashara yako ndivyo unavyoongeza kujulikana kwa biashara yako na kupata wateja wapya na wengi zaidi kwenye biashara yako.

Kupata Soko La Jipya La Bidhaa zako

Kama una bidhaa mpya dukani au huduma mpya basi inapaswa uifanyie matangazo ili uitafutie soko lake hivyo matangazo yanasaidia katika kutafuta soko la bidhaa mpya kwenye biashara yako.

Kuwashinda Wapinzani Wako

Matangazo yanasaidia kuwazidi washindani wako kwa kuwavutia wateja wengi zaidi kuja kwako Unapofanya matangazo ndipo unapoongeza ushindani wako na hii husaidia kuwashinda wengine.

Kujenga Picha Nzuri Ya Biashara Yako

Matangazo hutengeneza uaminifu mzuri kwa mteja na kupelekea kuifanya biashara yako kuwa na Mvuto mzuri kwa jamii.

Njia za Kutangaza Biashara

Matangazo Ya T-shirt

Unaweza ukaamua kununua tisheti zisizo nz maandishi na kisha kuziprint nembo ya biashara yako au kuchapisha maneno ya kutangaza biashara yako.

Pia Unaweza ukaaamua kuzigawa hizi tisheti kwa watu mbalimbali na kuwapa wafanyakazi wawe wanazivaa au kuzitoa kama zawadi tu.

Matangazo Ya Vipeperushi

Unaweza ukaamua kumpa kazi Graphic designer ambaye ana utaalamu zaidi kutengenezea vipeperushi vyenye kuvutia kwa ajili ya kutangaza biashara yako.

Vipeperushi Vya matangazo yako unaweza kuvigawa kwenye Vituo vya Usafiri, Mabasi, Mashuleni na Sehemu zingine Ambazo vitawafikia wateja wako kwa urahisi.

Matangazo Ya Udhamini wa Mambo

Hapa Biashara yako itadhamini Event, Blog, Video Clip, Michezo na Vitu vingine vingi na Kisha kupewa nafasi ya kujitangaza kupitia udhamini huo.

Matangazo Ya Blog

Unaweza ukaongea na wenye websites au blog ambazo hutembelewa na wasomaji wengi kwa siku. Kisha ukawalipa kwa kununua sehemu za matangazo ndani ya blog hizo.

Matangazo Ya Social Media

Unaweza ukatumia mitandao mbalimbali ya kijamii kuweza kutangaza biashara yako. Kwa mfano unaweza ukajitangaza Kupitia Facebook, Instagram au mitandao mingine ya kijamii ambayo inakupatia nafasi ya kukutana na wateja wako.

Matangazo Ya Magazeti

Magazeti yana sehemu za kwenye kurasa ambazo zimetengwa kwa ajili ya matangazo Hivyo Unaweza ukatumia sehemu hizo kwa kulipia matangazo na kuwafikia wateja wako.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

2 Comments
  1. Asante sana leo nimefahamu jinsi nitakavyo tangaza biashara yangu.

Leave a reply