Mambo Ya Kuzingatia Unapofanya Biashara Mtandaoni

Vitu vya kuzingatia unapofanya biashara mtandaoni Tanzania ni muhimu kufahau mapema kwasababu Kufanya biashara kwenye mtandao ni jambo lenye faida na changamoto zake.

Unaweza ukawa na bidhaa nzuri sana lakini ukumbuke kuwa kila siku kunaanzishwa tovuti za kuuza bidhaa mtandaoni.

Haijalishi kuwa wewe ni muuzaji wa bidhaa wa siku nyingi au wa karibuni, ni wazi kuwa utakutana na changamoto kadha wa kadha.

1. Jitahidi Kuepuka Kukosa Huduma Kwa Wateja

Ni rahisi mtu kukaa dukani kwake siku nzima ili kuwahudumia wateja; lakini unaona hakuna umuhimu wa kukaa karibu na wateja wake wa kwenye mtandao.

Kumbuka hawa ni wateja kama wateja wengine, wanaweza kuwa wana maswali, maombi au mapendekezo wanayotaka kuyafikisha kwako.

Wateja watakufikia vipi na wewe hujaweka mfumo mzuri wa huduma kwa wateja? Je watanunua tu vitu kwa sababu unapenda wanunue? La hasha! Kutokana na kosa hili hutoweza kupata wateja na kufanikiwa katika biashara yako.

2. Jitahidi Kuepuka Kutengeneza Website Mbaya

Katika jambo muhimu kwenye biashara ya kwenye mtandao ni tovuti iliyotengenezwa au kusanifiwa vizuri. Watu wengi hutengeneza tovuti mbaya ambazo siyo rafiki kwa wateja na vifaa vyao.

Hili huwagharimu wengi kwa kupoteza wateja wengi. Zingatia mambo haya katika kutengeneza tovuti nzuri ya kufanyia biashara ya kwenye mtandao:

  • Hakikisha inaweza kuonekana vyema kwenye vifaa vyote kama vile simu, tablet na kompyuta.
  • Hakikisha ina mfumo mzuri wa viungo (Menu and Navigation) kwa njiaa hii mteja ataweza kuperuzi vyema kwenye tovuti yako.
  • Hakikisha inasehemu ya utafutaji.
  • Boresha tovuti kwa ajili ya injini pekuzi (Search Engine Optimization – SEO)

Ukizingatia mambo haya tovuti yako itakuwa nzuri kwa wateja na kukufanya kupata mauzo zaidi.

3. Jitahidi Kuepuka Ufafanuzi Mbovu wa Bidhaa

Hakuna mtu anayenunua kitu ambacho hajakifahamu vizuri au kukiona. Kosa la ufafanuzi au maelezo duni ya bidhaa limewafanya wateja wengi kutonunua bidhaa za wafanya biashara wengi.

Hakikisha bidhaa ina picha nzuri na maelezo ya kutosha kumfanya mteja aielewe bidhaa yako ili awe tayari kuinunua.

Kwa mfano mtu unaweka picha ya bidhaa fulani kwenye tovuti au mtandao wa kijamii bila hata maelezo yoyote, je unafikiri kwa sababu umeiweka kama cover au profile picture ndiyo itanunuliwa? Ni lazima watu wapate maelezo ya kutosha na jinsi bidhaa husika itakavyowasaidia ndipo watainunua.

4. Jitahidi Kutumia Mitandao Ya Kijamii

Wafanya biashara wengi hawajui umuhimu wa mitandao ya kijamii wala matumizi yake kwenye biashara zao.

Biashara ya kwenye mtandao inahitaji ufahamu matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ili kupata wateja wengi zaidi kwa ajili ya bidhaa zako.

Hakikisha unawajulisha watu jinsi bidhaa zako zitakavyotatua matatizo yao pia usisahau kuwajulisha punguzo (offer), bei na njia ya kuzipata bidhaa zako.

5. Jitahidi Kuepuka Kutokufahamu Wateja na Soko Lako

Kufahamu wateja na soko ni hatua mojawapo ya kukuwezesha kukuza mauzo ya bidhaa zako. Hebu fikiri unatangaza bidhaa za urembo za wanawake kwenye group la wa Whatsapp, je utapata wateja kweli? Naamini hutopata wateja jinsi ipasavyo.

Ni wazi kuwa ni muhimu ujue soko lako liko wapi na ulilenge ipasaavyo.

6. Jitahidi Kuepuka Mfumo Mbovu wa Kulipia Bidhaa

Mara nyingi unapouza vitu kupitia mtandao wateja watalipia bidhaa zao moja kwa moja, pia watafahamu jisi watakavyopata bidhaa husika.

Wauzaji wengi hawaweki mfumo rahisi kwa wateja ili waweze kufanya malipo kwamfano tovuti za Afrika Mashariki tunategemea kuona njia za malipo kama vile M-Pesa, Airtel Money, Tigo pesa au MTN.

Pia ni lazima kuwe na mfumo mzuri wa kuwasafirishia au kuwafikishia wateja bidhaa zao. Kwa kufanya hivi utaaminika zaidi na kujiongezea wateja

7. Jitahidi Kutatua Matatizo Kuliko Kuuza Bidhaa

Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kuwa pesa ni matokeo ya kutatua shida za watu. Pamoja na kulenga kuuza bidhaa zako na kupata pesa, ni lazima kwanza uhakikishe unatatua matatizo ya watu kupitia bidhaa zako kwanza.

Ni muhimu pia kujenga imani kwa wateja kwa kuwapa garantii na punguzo (offer) kwa ajili ya bidhaa zako. Kwa kufanya hivi utaongeza imani ya watu kwenye bidhaa na biashara yako.

8. Jitahidi Kujitangaza Zaidi

Biashara ni matangazo Jinsi matangazo yalivyo muhimu katika biashara za aina nyingine, ndivyo ilivyo pia kwenye biashara ya kwenye mtandao.

Ni lazima utumie njia mbalimbali za kuzitangaza bidhaa zako, ukihusisha njia za bure na zile zakulipiwa. Kwa njiaa hii utawezakutambulika kati ya washindani wako, hivyo kufikia wateja wengi zaidi.

Kamwe usifanye kosa la kuupuuzia matangazo kwenye biashara ya kwenye mtandao kwani kuna ushindani mkubwa.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo