Mambo Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuomba Mkopo wa Biashara

Mambo Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuomba Mkopo wa Biashara ni muhimu kufahamu Kutokana na kipato cha watu wengi kutokutosheleza mahitaji yao, hujikuta wakilazimika kukopa.

Pia wapo waliofanikiwa sana kwenye mipango yao kutokana na mikopo, lakini wapo pia waliofilisika kutokana na mikopo.

1. Fahamu Uwezo Wako wa Kifedha

Ili upate na utumie mkopo vyema, ni muhimu ufahamu uwezo wako wa kifedha. Ikiwa uwezo wako wa kifedha ni shilingi milioni moja, ukikopa mkopo wa bilioni 1 hutoweza kuupata wala kuurejesha.

Hakikisha unatathimini kipato chako pamoja na uwezo wako wa kutumia pesa ili usije ukatumbukia kwenye madeni.

2. Andika Mpango wa Matumizi na Marejesho

Watu wengi hushindwa kupata mkopo au kurejesha mkopo kutokana na kutokuwa na mpango mzuri wa matumizi na urejeshaji wa mkopo.

Hakikisha kabla ya kukopa unaandaa mpango mzuri na unaotekelezeka na namna utakavyotumia pamoja na kurejesha mkopo wako. Usikope ndipo upange, bali panga ndipo ukope.

3. Fahamu Vizuri Kuhusu Riba

Benki ni taasisi zinazofanya biashara ili zipate faida; benki hufanya biashara hasa kwa kupitia mikopo. Ni muhimu kufahamu vyema kiwango cha riba utakachotozwa kutokana na mkopo uliokopa.

Watu wengi wameingia kwenye matatizo makubwa baada ya kujikuta wakikopa mikopo yenye riba kubwa sana. Hakikisha unafahamu riba utakayotozwa na utathimini kama utaweza kuimudu.

4. Fahamu Vizuri Muda wa Mkopo

Kadri mkopo unavyokuwa wa muda mrefu ndivyo na kiwango chake cha kulipa kwa mwezi huwa kidogo. Hivyo ni muhimu sana kuchunguza muda wa kurejesha mkopo ili uone kama unaweza kumudu kurejesha mkopo huo ndani ya muda husika.

5. Fahamu Vizuri Gharama za Mkopo

Mara nyingi mikopo huambatana na gharama nyingine kama vile gharama ya kuchakata mkopo, gharama ya kurejesha mapema zaidi, gharama ya kujiondoa mapema, n.k.

Ni vyema ukafahamu gharama hizi ili uone kama utazimudu vyema. Hakikisha waraka wa mkopo unaopewa unausoma na kuuelewa vyema kabla ya kuidhinishiwa kupokea mkopo ili kuepusha matatizo yoyote mbeleni.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply