Mambo Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanzisha Biashara Tanzania

Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanza kufanya biashara tanzania ili kupelekea kufanya biashara na kupata mafanikio katika biashara yako

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA BIASHARA

  • Tambua biashara gani inakufaa.

Kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya biashara fanya utafiti wa biashara gani inakufaa. Tumia muda wa kutosha kufanya uchunguzi na Ni muhimu kufanya kitu ambacho tayari unakifahamu.

  • Mpango wa biashara.

Watu wengi huanzisha biashara pasipo kuwa na mpango wa biashara. Hili ni kosa kubwa kwani kabla ya kuwekeza unapaswa kujiuliza unawekeza kwenye nini hasa? Utamuuzia nani? Lengo lako ni nini? Vipi kuhusu matarajio?

Hakikisha unaandika mpango wako wa biashara ili utakafungua mradi wako mpango huo ukuongoze kufikia malengo yako.

Kabla ya kufungua biashara ni lazima utambue soko lako Kabla ya kufungua biashara ya duka ni lazima kujua nani hasa ni mteja kwenye biashara yako.

Hupaswi kukurupuka kwani ushindani sokoni ni mkubwa hivyo unapaswa kuwalenga watu fulani. Fanya utafiti na tambua soko lako kabla ya kuwekeza kwenye biashara unayofikiria.

  • Jipange kifedha.

Hakikisha kuwa matumizi yako binafsi hayaingiliani na matumizi ya biashara Kuwa makini na matumizi yako ya fedha kwani biashara yako inaweza kuathirika moja kwa moja kama ukiendekeza matumizi makubwa kuliko kipato unachoingiza.

Wataalamu wanashauri kuwa na akaunti mbili za matumizi, moja kwa ajili ya biashara na nyingine ya matumizi binafsi ili kurahisisha mchakato mzima.

  • Usishindane na waliofanikiwa.

Usitumie muda mwingi kutaka kuwapiku wale ambao umewakuta kwenye soko la biashara. Jifunze kutoka kwao kwani wana ujuzi zaidi.

Waheshimu na jenga mahusiano mazuri ya kibiashara. Boresha biashara yako ili kuwavutia wateja.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

2 Comments
  1. Mimi baada ya kusoma vitu vya kuzingatia kabla ya kuanza biashara nikaamua kuanza kufanya biashara ya kuuza vyakula.

Leave a reply

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general