Dalili za Magonjwa Yanayoshambulia Nguruwe na Tiba Zake

Magonjwa yanayoshambulia nguruwe yana tiba pia ni mengi kama ilivyo kwa wanyama wengine yanavyotokea lakini kuna magonjwa katika ufugaji wa nguruwe lazima uyajue pamoja na tiba zake kwakua ndio yanayo jitokeza mara kwa mara

1. Ugonjwa wa miguu na midomo kwa nguruwe

Huu ni moja ya magonjwa ya nguruwe Ugonjwa huu huathiri midomo na miguu ya nguruwe Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.

Chanjo: Chanjo yake huitwa FMD VACCINATION nautolewa kila baada ya mwaka mmoja

Dalili: dalili zake miguu na midomo ya nguruwe inabadilika na pia nguruwe anadhoofika

Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.

2. Ugonjwa WA homa ya nguruwe

Ugonjwa huu unasambaa kwa kasi kama mmoja akiambukizwa wengine pia wataambukizwa na kufa

Dalili: nguruwe anakua na vidonda na vitu kama vibarango mwili mzima pia mdomo na masikio yanabadilika rangi nakua mekundu.

Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.

Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine kwa kua huu ni viral  disease

3. Ugonjwa wa mapafu kwa nguruwe

Huu ni moja ya magonjwa ya nguruwe ambayo Ushambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.

Dalili: nguruwe hukooa na kupumua kwa shida sana

Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.

4. Ugonjwa WA kimeta

Huu ni moja ya magonjwa ya nguruwe unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi

Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

6 Comments
  1. Asante kwa elimu hii ya ufugaji. Mimi ni mfugaji mpya ndio naanza niko arusha.
    Napenda taarifa mbalimbali na ushauri juu ya ufugaji wa nguruwe.

  2. Asante kwa maelezo yako siku zote dalili za magonjwa ya nguruwe zinatia hofu sana.

Leave a Reply to Kibona Cancel reply