Kilimo Cha Pamba Tanzania

Kilimo cha Pamba hulimwa nchini Tanzania na hukuzwa mikoa mbalimbali na pia pamba ndio hutumika kutengenezea uzi na nguo.

Pia mbegu za pamba hutumika kutengeza mafuta, mafuta ambayo tunatumia kupikia na mashudu ya mbegu yana kiasi cha protein ambayo mashudu hayo hutumika kama chakula kwa mifugo.

Hali Ya Hewa na Udongo

Kilimo cha Pamba hustawi vizuri katika maeneo yenye joto, kwa hapa tanzania hufanya vizuri katika mikoa ya kanda ya ziwa yaan chini ya 1400m kutoka usawa wa bahari mfano Mwanza, shinyanga na geita.

Kilimo cha Pamba huitaji kiasi cha mvua 25mm kwa miezi miwili ya kwanza, katika mwezi wa nne pamba huitaji kiasi cha mvua 75mm, na katika miezi inayo fuata pamba huitaji mvua ndogo ili kuwezesha pamba kukomaa

Pamba hustawi vizuri katika udongo wa aina nyingi, japo kua haiitaji ardhi inayo tuamisha maji, ila katika udongo wenye PH chini ya 5.0 pamba haistawi vizuri.

Aina za Kilimo cha Pamba

Aina nyingi za pamba ambazo hulimwa Tanzania zimefanyiwa utafiti na kugunduliwa ukiriguru, aina nyigi za ukiliguru huitwa UK au UKA variety mmbegu hizo hufanya vizuri zaidi katika mikoa ya kanda za magharibi

Aina nyingine zimetokea ilonga aina hizo nyingi huitwa IL mfano IL 85 Variety mbegu hizo hufanya vizuri katika mikoa ya mashariki.

Jinsi Ya Kupanda zao La Pamba

Andaa shamba la pamba kwa kutumia jembe la mkono, ng’ombe au tractor, kama unapanda maeneo yenye udongo mzito weka matuta kwa kufanya mistari ya contua.

Panda mbegu 6 hadi 10 katika kila shimo, nafasi hutegemea na eneo ulilopo na kama upo maeneo ya magharibi tumia nafasi 60cm x 15cm kama, kama unatumia matuta tumia nafasi 150cm na panda mistari miwili kila tuta.

Nafasi ya mistari ni 45cm na nafsi ya mimea ni 45cm na kama unapanda pamba katika mikoa ya pwani tumia 90cm x 30cm.

Jinsi Ya Kupalilia zao La Pamba

Mimea ya pamba inapofikisha urefu wa 10cm hadi 15cm unatakiwa kung’olea, kwa maeneo ya magharibi acha mmea 2 katika shimo na kwa mikoa ya pani acha mmea 1 katika shimo ng’olea mapema baada ya palizi ya kwanza.

Jinsi Ya Kupalizi Shamba La Pamba

Unatakiwa kupalilia pamba pale unapo taka kung’olea baadae unaweza kupalilia kadri na jinsi magugu yanavo ota shambani.

Katika mashamba makubwa ya pamba unaweza kufanya palizi kwa kutumia viua gugu, kiuagugu kinacho fanya vizuri ni diuron, na zingatia kusoma maelezo ya mtengenezaji kabla ya kutumia.

Mbolea Kwenye Kilimo cha Pamba

Kama mbolea ya samadi inapatikana unatakiwa kuweka mbolea mapema katika kipindi cha kuandaa shamba kama samadi.

Kama haipatikani unaweza kuweka 125kg ya single super phosphate katika shamba la ukubwa wa hekta moja kama mbolea ya kupandia.

Baada ya wiki 6 toka mda wa kupanda unaweka mbolea ya kukuzia yaani SA au CAN, tumia mbolea kiasi cha 125kg katika hecta moja ya shamba.

Zingatia kuweka mbolea baada ya kupalilia na kung’olea pamba.

Wadudu na Magonjwa Ya Pamba

Kilimo cha Pamba huathiliwa na wadudu wa aina nyingi sana mfano vitumba wa marekani, vitumba wekundu, vitumba wa awaridi, nematodes, mchwa na vidudu mafuta.

Pia kunanjia mbalimbali ya kuzuia wadudu hao, njia mojawapo ni kama vile kutumia viuadudu, pulizia dawa angalau wiki mbili mara sita, pulizia dawa kuanzia wiki 6 toka kupanda.

Dawa za kuua wadudu ni kama carybryl na endosulfuan.

Magonjwa yanayo shambulia pamba ni kama vile bacteria bright, fulsalium wilt na vertllium wilt tumia dawa za fungus na pia zingatia kuandaa mbegu zinazo staimili magonjwa.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo