Kilimo Cha Mapapai Tanzania

Kilimo cha Papai ni kilimo kizuri sana hapa Tanzania na mapapai ni moja ya matunda ambayo ni maarufu pia ni mazuri sana kwa afya.

Ekari moja ya papai inachukua miche 1000-1200 kwa maana ya mita mbili kwa mbili kutoka mti hadi mti na hii ni kwa ile mbegu fupi.

Ukilima kwa kufuata utaalamu ni kwamba mti mmoja wa papai unaweza kutoa matunda 86 hadi 100 kwa msimu.

Kutoka kupandikiza shambani hadi kuanza kuvuna mavuno ya kwanza, papai zinachukua miezi nane hadi kumi tu.

ikiwa unamwagilia papai ni tunda lisilo na msimu, yaani unavuna mfululizo.

Mti mmoja unatoa matunda 86 hadi 100 sasa kwa ajili ya kustandadaizi tuchukulie kwamba mti umekupatia matunda 80 pekee.

Mahitaji Ya Kilimo Cha Mapapai

Hali ya hewa inayofaa kwa mipapai ni ya tropic ambayo haina baridi kali na joto kiasi.

Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu.

Kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia inafaa.

Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi.

Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa.

Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti na mboga mboga yanaweza kulimwa.

Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike na yenye jinsia zote (multiplesex/hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana.

Mbegu Nzuri za Kilimo Cha Mapapai

Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja.

Papai lililokomaa linaweza kutumika kama mbegu.

Jinsi Ya Kuotesha Mbegu za Papai

Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla.

Mbegu zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 chini ya udongo wenye rutuba au pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 na 27 na itachukua kati ya wiki 1 mpaka 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 au 3.

Panda mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na fangasi.

Jinsi Ya Kuotesha Moja Kwa Moja

Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa.

Panda mbegu 3 mpaka 5 kila shimo maana miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume

Jinsi Ya Kuhamisha Miche Kutoka Kwenye Kitalu

Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 – 40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 – 60.

Mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha.

Jinsi Ya Kuipunguza Mipapai

Baada ya miezi 3 mpaka 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume.

Mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 au 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe

Jinsi Ya Kurutubisha Udongo

Weka kiasi cha kilo 2 mpaka 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

Jinsi Ya Kuzuia Magugu

Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu.

Uangalizi wa Shamba La Mapapai

  • Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako.
  • Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
  • Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu.
  • Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike.
Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo