Kilimo Cha Maboga Tanzania

Kilimo cha Maboga ni kilimo maarafu kwa Tanzania pia maboga ni zao ambalo mmea wake unakuwa kwa kutambaa na ni la mviringo na rangi yake ni ya njano inayoelekea kwenye rangi ya chungwa au rangi ya kijani.

Asili Ya Kilimo cha Maboga

Asili ya maboga ni Amerika kaskazini, maboga yamekuwa yakipandwa kwaajili ya biashara na kwaajili ya chakula.

Kwa sasa maboga yamekuwa yakilimwa maeneo mbalimbali duniani na Mataifa yanayozalisha maboga kwa wingi ni Marekani (USA), Canada, Mexico, India, and China.

Hali Ya Hewa na Udongo

Maboga yanahitaji joto la wastani kutoka kwenye jua, pia eneo ambalo halituamishi maji udongo wake uwe na pH kati ya 6.0 – 6.8.

Pia udongo uwe na joto inchi tatu (sm 7.6) kushuka chini angalau nyuzi 60 °F (15.5 °C), maboga yatadhoofika kama maji yatakosekana.

Utayalishaji wa Shamba La Maboga

Shamba la maboga litayalishwe kwa umakini bila kuwa na sehemu ya kutuamisha maji maana mmea wa maboga na maboga yenyewe hutambaa chini pia changanyia mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha shamba la maboga.

Utayalishaji wa Mbegu za Maboga

Mbegu za maboga zinatoka ndani ya maboga, kuna mbegu zilizoboreshwa na za asili, andaa mbegu mapema wiki moja au mbili kabla ya kupanda.

Upandaji wa Mbegu za Maboga

Maboga hupandwa kwa kufukia mbegu sentimita 1 au 2 chini ya udongo , panda mbegu 2 kila shimo. Pia panda umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 2 kutoka mstari hadi mstari.

Matandazo Ya Maboga

Kilimo cha Maboga Kwasababu ni zao linalotambaa basi lazima tuangalie namna ya kutandaza, weka nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika ardhi.

Baada ya miche ya maboga kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako.

Mbolea Nzuri za Maboga

Katika matumizi ya mbolea yanatofautiana kutokana na mbegu za maboga, Lakini tumia mbolea za asili (samadi au mboji) ili kuongeza rutuba kwenye udongo

Ukihitaji kutumia mbolea za viwandani weka kiasi kidogo sana, labda eneo hilo kama hakuna rutuba, mbolea ya NPK inaweza tumia.

Upaliliaji wa Shamba La Maboga

Palilia shamba la maboga nyasi zinapoanza kuota, pia safisha shamba la maboga ili kuondoa wadudu pia Shamba la maboga linatakiwa liwe na unyevunyevu kila mara ili maboga yaweze kustawi vizuri yasidumae.

Uvunaji wa Maboga

Maboga hukomaa baada ya siku 95 mpaka 120, ili kujua kuwa boga lako limekomaa unaangalia kikonyo, kikonyo cha boga kinapoteza maji na kinaanza kuwa kikavu.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo