Jinsi Ya Kutengeneza Pesa Online Tanzania

Jinsi ya kutengeneza pesa online

 • Kuanzisha blogu

Kama wewe ni mwandishi unaweza kutengeneza pesa online kwa kuanzisha blogu yako na kuandika makala au habari mbalimbali Unachotakiwa kuzingatia ni mahitaji ya walengwa wako na kuwapa kile wanachotaka.

Kama wewe ni shabiki mkubwa wa masuala ya mpira basi blogu yako ihusiane na michezo. Kupitia blogu unaweza kujiingizia kipanto kutokana na matangazo na idadi ya watu wanaopitia habari zako.

 • Kuwa meneja wa mitandao ya kijamii

Biashara nyingi hivi sasa zimejikita kwenye mitandao ya kijamiii ili kuwafikia watu wengi kwa urahisi zaidi. Ikiwa una ujuzi wa kutosha wa mitandao kama Facebook na Instagram unaweza kutumia fursa hiyo kuingiza kipato kwa kusimamia mitandao ya biashara na kutangaza kampuni au taasisi huzika.

 • Kutoa mafunzo

Badala ya kutumia muda mwingi kutafuta ajira unaweza kutumia nafasi hiyo kutoa mafunzo online ya kitu ambacho una uelewa na ujuzi nacho kupitia mitandao mbalimbali.

Mfano kama wewe ni mpishi mzuri unaweza kufungua chaneli ya online ambayo itatoa mafunzo kuhusu mambo ya mapishi pia Unaweza kufundisha kuhusu ujasiriamali, urembo na hisa

 • Kutoa huduma za SEO

Sekta ya SEO imeendelea kukua kwa kasi duniani kote. Kama wewe ni mtaalamu unaweza kutoa huduma hii kwa makampuni na vyombo vya habari na kujitengenezea kipato.

 • Kufungua chaneli Youtube

Katika ulimwengu huu wa digitali mtandao kama Youtube hutembelewa na maelfu ya watu kila siku Unaweza kutumia fursa hiyo kuanzisha chaneli yako na kuweka video zako online.

Utakapopata wafuasi wa kutosha unaweza kuingiza fedha kwa kutumia Google Adsense ambayo hutumika kuweka matangazo kwenye video.

 • Kuanzisha Podcast

Podcasting ni njia nyingine nzuri kwa wajasiriamali kutengeneza hela online Unaweza kuanzisha podcast yako mwenyewe na kuuza matangazo yako na ya wafadhili walio karibu na maudhui yako.

 • Kuuza bidhaa eBay au Etsy

Kama una bidhaa unazotaka kuweka sokoni anzisha duka lako online kwenye majukwaa kama eBay ili kuuza bidhaa zako.

Kama wewe ni mtaalamu wa kutengeneza bidhaa za mkono mtandao wa Etsy ni sehemu nzuri kwa ajili ya kuuza vifaa hivyo. Unaweza kuanzisha duka lako hapo na kufanya biashara.

 • Uhariri

Watu binafsi na wafanyabiashara pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wana uhitaji mkubwa wa wahariri. Ikiwa wewe ni mtu makini kwenye masuala haya unaweza kufanya kazi hii online na kupata pesa nzuri.

 • Kuanzisha mtandao wa matangazo

Unaweza kuanzisha mtandao maalum wa online ambao unalenga kutangaza biashara binafsi pamoja na zile za mashirika za mtandaoni na kutengeneza fedha kupitia matangazo hayo.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

6 Comments
 1. Napenda sana Kufanya kazi na Kutengeneza pesa online

 2. Asante na mimi nitafungua account yangu ya biashara.

 3. Asante sana nimekuelewa sana

Leave a reply

Wauzaji
Logo