Jinsi Ya Kupunguza Matumizi Ya Umeme Tanzania

Kupunguza matumizi ya umeme Tanzania kunaweza kuokoa fedha nyingi ambazo zingepotea kwa kulipia gharama zisizo na sababu za matumizi ya umeme.

1. Jitahidi kuzima taa na vifaa usivyo vitumia

Mara nyingi umeme mwingi hupotea kutokana na kuacha vifaa mbalimbali vikiwa vimewashwa bila sababu. Si jambo la kustajabisha watu kusahau taa za nje ya nyumba hadi saa sita mchana.

Jitahidi kuzima vifaa kama vile redio, televisheni au kompyuta vikiwa vimewashwa mchana au usiku kucha bila sababu ya msingi.

Jifunze kuzima taa na vifaa vingine vinavyotumia umeme wakati ambapo havihitajiki au havina umuhimu ili kookoa matumizi yasiyo ya lazima ya umeme.

2. Jitahidi kutumia nishati mbadala

Kuna watu hufikiri kuwa kutumia nishati kama vile umeme kupikia ndiyo kuwa wa kisasa zaidi; lakini ukweli ni kuwa huku ni kujiongezea gharama zisizokuwa na sababu.

Matumizi ya gesi na umeme jua ni nafuu zaidi kuliko kutumia umeme.

Mambo unayoweza kufanya hapa:

  1. Tumia gesi kupikia badala ya umeme kwani gesi ni nafuu zaidi.
  2. Tumia taa na vifaa vya umeme jua (solar) pale inapowezekana.

Kwa kufanya hivi utaweza kuokoa nishati ambayo ingepotea katika matumizi ya umeme kwenye kila kifaa.

3. Jitahidi kuondoa vifaa vya zamani

Sera za dunia zimebadilika katika jitihada za kutunza mazingira. Vifaa vinavyozalishwa hivi leo, vingi hutengenezwa kwa kuzingatia kulinda mazingira kwa kuokoa matumizi ya nishati.

Hivyo ni vyema ukaondoa vifaa vya zamani kama vile televisheni, kompyuta za mezani, redio, taa au jokofu ambavyo vimetengenezwa kwa teknolojia ya zamani inayotumia umeme mwingi.

4. Jitahidi kuzima au punguza matumizi ya friji

Friji ni moja kati ya vifaa vinavyotumia kiwango kikubwa cha umeme. Kupunguza matumizi ya Friji ina maana kuwa ni kubadili kiwango cha matumizi ya umeme.

Unaweza kuwasha jokofu kwa muda fulani tu na si kwa siku nzima pia unaweza kuepuka kufungua friji mara kwa mara ili kutunza ubaridi ndani ya frijiili lisiwashwe mara kwa mara.

5. Jitahidi kutumia pasi vizuri

Ni vizuri kupasi kila nguo unayoivaa, lakini matokeo yake kwenye matumizi ya nishati siyo mazuri. Watu wengi hawafahamu kuwa umeme mwingi sana hupotea wakati wa kupasi na kuwasababishia kulipa bili kubwa za umeme.

Hata hivyo, yapo mambo unayoweza kufanya ili kuokoa matumizi ya umeme kwa kutumia vizuri pasi ya umeme.

  1. Nunua pasi nzuri yenye viwango na ubora stahiki.
  2. Nunua nguo zisizohitaji kupasiwa kila mara au kupasiwa kabisa.
  3. Pasi nguo kwa pamoja. Ni vyema kupasi nguo tano kwa wakati mmoja kuliko kupasi kila siku nguo moja, kwani utapoteza umeme mwingi kupasha pasi moto mara kwa mara kila siku.
  4. Usifue nguo kwa maji ya moto sana. Kufua nguo kwa maji ya moto sana husababisha nguo kujikunjakunja sana, hivyo kuhitaji umeme mwingi kuzinyoosha.
  5. Pasia mahali sahihi. Unapopasia sehemu kama sakafuni ni dhahiri kuwa joto jingi litapotea kwa kupasha joto sakafu, hivyo kupelekea matumizi makubwa ya umeme. Ni vyema ukapasia kwenye meza maalumu ya kupasia au kwenye meza iliyofunikwa kwa kitambaa.
  6. Pasi wakati kuna umeme wa kutosha. Inawezekana mahali unapoishi kiwango cha umeme hupungua wakati fulani ni vyema kupasi wakati umeme upo wa kutosha ili pasi isivute umeme sana na kupelekea matumizi makubwa ya umeme.

6. Jitahidi kumia taa zenye energy server

Hivi leo sokoni kuna aina mbalimbali za taa  za umeme, lakini siyo zote zinafaa kwa matumizi yako. Balbu za zamani hutumia umeme mwingi zaidi huku zikikupa matokeo duni.

Leo zipo taa zinazojulikana kama “Energy Severs” ambazo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia inayookoa nishati huku zikikupa matokeo mazuri zaidi.

7. Jitahidi kukagua mfumo wa umeme

Mfumo duni wa umeme (wiring) kwenye nyumba yako unaweza kusababisha upotevu mkubwa wa umeme. Kwa mfano ikiwa umeme unavuja kimakosa na kuingia kwenye waya wa aridhini (earth), umeme mwingi utapotea kwenda kwenye ardhi bila wewe kujua.

Unaweza kumtafuta fundi au mtaalamu wa masuala ya umeme wa nyumba, ili aweze kukusaidia kukagua mfumo wako na kuhakikisha kuwa hakuna sehemu inayovujisha na kukupotezea umeme.

8. Jitahidi kupunguza matumizi ya feni na Ac

Mara nyingine kutokana na mazingira ya joto mtu anahitaji kutumia feni (pangaboi) au kiyoyozi ili kukabili joto.

Ni vyema ukafahamu kuwa vifaa hivi huhitaji umeme ili kujiendesha hasa kiyoyozi huhitaji umeme mwingi ili kufanya kazi.

Pamoja na hilo, yapo mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kuokoa umeme unaotumiwa na kiyoyozi na feni.

  1. Tumia njia za asili za kupambana na joto. Unaweza kufungua madirisha na milango kama inawezekana ili kukabili joto badala ya kutumia kiyoyozi na feni.
  2. Unapowasha kiyoyozi funga madirisha na milango ili chumba kiwe na baridi haraka na idumu kwa muda mrefu zaidi.
  3. Tumia zaidi feni kuliko kiyoyozi ili kupunguza matumizi makubwa ya umeme yanayotumiwa na kiyoyozi.
  4. Zima feni na kiyoyozi pale ambapo havina ulazima.
Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply