Jinsi Ya Kupata Wazo Zuri La Biashara

Njia za kupata wazo la biashara kwa Tanzania kama ukizifuata unaweza kujikuta umepata wazo bora la biashara na lenye faida kwa Tanzania.

Namna Ya Kupata Wazo la Biashara

1. Angalia Uhitaji wa Watu

Kabla hujaanza Biashara yako angalia uhitaji wa watu ambako unataka kuanzisha Biashara yako. Jiulize ni Bidhaa au huduma gani inahitajika katika sehemu unapo taka kufungua Biashara hiyo.

2. Fanya Utafiti wa Biashara

Fanya utafiti juu ya mambo mbalimbali ikiwemo ukubwa wa Uhitaji na kipato cha watu ili kuweka usawa katika Bidhaa au Huduma yako kulingana na Vipato cha wateja wako.

Pia Fanya utafiti juu ya upatikanaji wa vitendea kazi (Materials).

3. Ipende Biashara Unayotaka Kuanzisha

Hauwezi kuanzisha Biashara yoyote tu eti kwa sababu una mtaji kivyovyote unaweza kujikuta umepata hasara na huifanya kwa kuipenda.

Kitu kitoke moyoni katika kukifanya, usipo kuwa na hisia na Biashara unayo hitaji kuanzisha utajikuta haina ule msukumo wenyewe katika kuikuza na kuiendeleza Biashara hiyo.

4. Angalia Gharama za Uendeshaji wa Biashara

Lazima utambue katika kuanzisha na kufanya Biashara yoyote kuna gharama ambazo huwa zina mlazimu mfanyabiashara kuzigharimia katika kuendesha Biashara yake. Gharama hizo zinaweza kuwa za moja kwa moja au ambazo sio za moja kwa moja.

5. Angalia Ushindani wa Biashara 

Ushidani Siku zote ndio ambao hutofautisha kati ya mfanya Biashara mkomavu na mbunifu na ikiwa unataka Kuanzisha Biashara katika mazingira ya ushindani basi jitahidi sana kujiweka tofauti na wafanya Biashara wenzako.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo