Jinsi Ya Kupata Mtaji wa Biashara Tanzania

Jinsi Ya Kupata mtaji wa biashara tanzania ni Moja kati ya changamoto kabla ya kuanza kufanya biashara au kuanzisha biashara yoyote Katika kipengele hiki naenda kujadili changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye biashara.

Jinsi Ya Kupata Mtaji wa Biashara

1. Tumia akiba zako kama mtaji, au anza kuweka akiba.


Kama kuna akiba zozote ambazo umekuwa unajiwekea kwa muda unaweza kuzitumia kama mtaji wa kuanzia biashara Kama huna akiba yoyote anza sasa kujiwekea akiba na jipe muda unaohitaji ili kufikisha kiwango cha mtaji unachotaka.


2. Chukua kazi hata yenye maslahi kidogo.


Kama ndio umemaliza shule na hujapata ajira na pia huna mshahara wa kuanzia nakushauri uchukue kazi yoyote unayoweza kupata hata kama ina maslahi kidogo. Lengo lako litakuwa ni kukusanya mtaji na hivyo utaifanya kazi hiyo kwa kipindi fulani na kisha kuachana nayo. Inabidi ukubali kuteseka kwa muda kidogo ili uweze kufika kule unakotazamia. Sasa kama utaniambia kwamba wewe ni msomi na kuna kazi huwezi kufanya, nitakuambia uendelee kuimba tatizo ni mtaji.


3. Anza kidogo.


Unapoanza biashara hasa pale unapoanzia sifuri ni vigumu sana kuweza kupata kiasi chote cha fedha unachohitaji. Unaweza kuanza kidogo na baadae ukaendelea kukua na pia kujifunza. Jua ni kiasi gani unahitaji kama mtaji na gawa kwenye kiasi kidogo ambacho unaweza kuanzia. Ukisema usubiri mpaka upate kiasi kikubwa unachofikiria itakuchukua muda mrefu sana na baadae utakata tamaa.


4. Ungana na mwenzako mwenye mawazo kama yako.


Unaweza kuungana na mwenzako au wenzako wenye mawazo kama yako na mkaunganisha fedha kidogo mlizo nazo na kuzifanya kama mtaji ili kuweza kuanza biashara. Hii ni njia nzuri sana ya kuweza kuunganisha mitaji kidogo ambayo unaweza kuitumia na ukafikia mafanikio makubwa.

5. Uza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa navyo ili kupata mtaji.


Kama unataka kuanza biashara ila huna mtaji, nakushauri uuze vitu vingi ambavyo ulinunua ukiwa masomoni ambavyo kwa sasa hauna uhitaji mkubwa navyo ili kupata mtaji, biashara yako itakurudishia na zaidi. Ukipiga mahesabu ya haraka haraka unaweza kupata kiasi fulani cha fedha kinachotosha kuanzia kama utauza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa kwa sasa.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

4 Comments
  1. Jamani Mimi ni chinga wa urembo nahitaji nifanikiwe kupata mtaji wa biashara nitumie mbinu gani?

    • Fuata Njia nilizoziandika pia Kumbuka ni watu wengi sana wanawaza jinsi ya kupata mtaji wa biashara kwa Tanzania kwaio usikate Tamaa na muombe mungu na pia anza na hiko hiko Kidogo ulichonacho.

      Kwasababu kwenye ujasiriamali Ukishindwa Kujaribu Basi utakuwa Unajaribu Kushindwa.

  2. Na mimi nikipata mtaji nitajitahidi nimiliki duka dogo la rejareja lenye kila kitu

Leave a reply

Wauzaji
Logo