Jinsi Ya Kupata Mafanikio Katika Maisha

Kuna mambo mengi umekuwa ukijiuliza ni kwa namna gani utajikwamua katika hali ngumu za kimaisha ila kuna njia mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia na kutoka kimaisha.

Zifuatazo ni mbinu ambazo unaweza kuzitumia ili uweze kufanikiwa katika mambo yako.

1. Weka malengo ambayo yatakuwa mwongozo wako.

Siku zote mtu ambaye anataka kufanikiwa katika maisha lazima kujiwekea malengo na njia ya kufikia malengo hayo, kwa kufuuta malengo hayo itakusaidia kukuongezea juhudi na akili ya ziada ambayo itakupa nafasi kubwa ili uweze kufikia malengo yako.

Kwa mfano katika biashara weka mikakati ya kufanya ili uweze kufanikiwa kibiashara.

2. Jiamini katika kufanya mambo yako. 

Kitu ambacho watu wengi wanakwama katika kufanya mambo yao ya kimaendeleo wanashindwa kujiamini wanapo kutana na changamoto katika biashara na maisha.

Ni vyema sana kujisemea kila siku “NAWEZA kwani walio weza wao wananini?”  hii itakufanya uwe mwenye juhudi katika maisha yako yote.

3. Usiogope kujaribu. 

Inapo tokea fursa ya kimaendeleo usikae nyuma changamkia fursa tena kuwa mstari wa mbele kwa mfano kwa mfanyabiashara inapo tokea tenda ya kusambaza bidhaa yako usiogope kwa kuhofia hasara au ukiona biashara unayo ifanya haina matunda jaribu nyingine utatoka tu!

Pia kwako mwanafunzi ikitokea wanafunzi kadhaa wanahitajika kwa ajiri ya jambo flani penda kuongeza maarifa kwa kuhudhuria semina pia za kimaisha kwani ni bora kujaribu kuliko kutojaribu kabisa ili usije kuanza kujilaumu wengine wakifanikiwa.

4. Jipende.

Katika kujipenda ni vile unavyo jijali, kujiheshimu, kujithamini na kujilinda hasa kiafya, siku zote afya ndio msingi wa maendeleo kwani bila afya bora shughuri mbalimbali zitakwama hivyo kukuludisha nyuma kimaendeleo.

Mtu ambaye anajiheshimu ataheshimika na watu na jamii kwa ujumla inayo mzunguka hii itamfanya kuwa na mahusiano mazuri na jamii yake inayomzunguka  hivyo ni rahisi kwake kupata fursa kutoka kwa watu na kuaminika.

5. Usikate tamaa.

Unapo kwama katika mambo yako chukulia kama changamoto tu na penye changamoto ndio penye mafanikio kwani hivyo changamoto yoyote ina suruhisho lake.

Tafuta msaada wa kimawazo namna gani utakabiliana na changamoto hiyo kwa waliofanikiwa “penda kujifunza kwa waliofanikiwa”.

6. Kuwa mwaminifu kwa watu. 

Mbinu nyingine ni kuwa na uaminifu na watu wanao kuzunguka katika maisha yako ya kila siku hii itakufanya wakuamini na kuona kuwa wewe ni mtu muhimu katika maisha yao.

Uaminifu huleta Upendo kati ya watu, na mahusiano mazuri kwa mfano mfanya biashara kuwa mwaminifu kwa wateja wako.

Wewe mwenye mahusiano kuwa mwaminifu kwa mwenza wako ili kudumisha upendo wenu hii itakuondolea mawazo yasiyo ya lazima (free stress) hivyo utafanya mambo yako kwa ufanisi mkubwa.

7. Ongeza ujuzi wa vitu mbalimbali.

Kuna njia Nyingi za kuongeza ujuzi kama vile kujisomea vitabu, Makala zinazo husiana na jambo ambalo unapenda kulifahamu kwa undani katika mitandao, mitandao ya kijamii kama vile youtube, facebook na twitter.

Pia tafuta Makala za kibiashara, elimu, mahusiano, siasa, jamii na maendeleo.

8. Mshirikishe MUNGU wako katika mambo yako. 

Hili nalo ni jambo muhimu sana katika mafanikio yako kwa kuwa itakuongezea kujiamini, utakuwa na Amani na huta kuwa na wasiwasi wa kushidwa kamwe.

Mshirikishe katika matatizo na changamoto unazo kutana nazo, kwa mfano unapo kosa msaada Mungu pekee ndio msaada wako.

9. Zingatia muda.

Katika kutimiza malengo zingatia ni lini au mda gani umepanga kutimiza lengo hilo kwa kuhakikisha kila lengo unalitimiza kwa mda mwafaka kwani “muda ni mali”

Hivyo usipoteze mda wako kwa jambo au mambo ambayo hujapanga kuyafanya labda kama kuna ulazima wa kufanya jambo hilo kwa wakati kama huo.

10. Fuatilia kwa kina malengo yako. 

Baada ya hayo yote nipende kusema kuwa lazima ufanye tathimini ya malengo uliyo jiwekea ya siku, wiki, mwezi na mwaka na kila mwisho wa mda wa lengo hilo unapofika.

Kufanya Tathimini kuta kusaidia kujua wapi umekwama, nini ufanye ili usikwame tena na kipi ufanye kuongeza mafanikio yako.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

4 Comments
  1. Naamini ipo siku nifanikiwa katika maisha

  2. Nimependa mlivyompa NAFASI MUNGU WETU MAANA YEYE NI mpaji wa vyote anakupa NAMNA ya kuvitumia visije vikakudhuru.

Leave a reply

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general