Jinsi Ya Kupanga Malengo Kwenye Maisha

Kupanga malengo kwenye maisha ni jambo muhimu na kama ukiamua kuanza unaweza kupanga malengo leo na kuhakikisha kuwa kesho inakuwa nzuri.

1. Jitahidi Kupanga Malengo Kuhusu kesho

Kuwa na mpango wa kesho leo kutakuwezesha kufanya mambo kwa kutegemea mwongozo na mpangilio uliopo badala ya kuamka na kufanya chochote kinachokuja mbele yako.

Panga mambo ambayo unatakiwa kuyakamilisha kesho kwa kutegemea umuhimu wake.

2. Jitahidi Kufiikiri Kwa Mapana

Ni vyema ukafahamu kuwa ni wapi ulipo leo na ni wapi unapotaka kwenda. Ni vyema ukatenga muda ukabainisha lengo lako la mbeleni kama unataka kuwa msanii mkubwa, mwandishi, rubani, daktari au mwanasiasa basi bainisha.

Hili litakusaidia kukuongoza kurudi kwenye lengo pale unapokuwa umeliacha. Ni vyema kila siku ukahakikisha unafanya kitu kwa ajili ya kulikaribia au kufikia lengo lako.

3. Jitahidi Kutengeneza Plan B

Maisha ni kama fumbo, yale uliyoyapanga leo yanaweza kesho yasiwe kama ulivyoyapanga. Hivyo ni vyema ukawa na mpango wa pili au mbadala pale ambapo mpango wa awali utakwama.

Hili ni jambo ambalo watu waliofanikiwa na werevu (smart) hulizingatia sana kwani wanajua mpango mmoja ukikwama watatumia mpango wa pili.

4. Jitahidi Kutambua Mafanikio Yako

Ni vyema ukatenga muda kutambua mafanikio uliyoyapata hata kama ni kidogo. Ni kweli kuwa hakuna mtu anayesema nimeridhika na mafanikio hivyo sitaki kufanikiwa tena, lakini ni vyema ukatambua mafanikio unayoyapata.

Kutambua mafanikio ambayo umebarikiwa kuyapata kutakupa hamasa ya kufanya bidii zaidi ili kuyafikia mengine makubwa na mazuri zaidi.

5. Jitahidi Kutambua Nguvu Yako Unayoitumia

Mara nyingi tumezungukwa na upinzani kutoka kwa watu na mazingira yanayotuzunguka. Inawezekana hakuna anayekuthamini, kukuunga mkono au hata kukutia moyo.

Jifunze kuepuka watu na mazingira haya ili kulinda nguvu yako ambayo ungeweza kuitumia kufanya vitu vyenye tija zaidi kwa jili ya leo na kesho.

Kama wanakusema, acha waseme; kama wanakudharau, waache wakudharau wewe tazama malengo yako tu, ipo siku watakuelewa.

6. Jitahidi Kuiona Kesho Kwa Mafanikio

Mara nyingi watu huona magumu kiasi cha kutoamini kuwa kunaweza kukatokea nuru kesho. Jifunze na jizoeze kuiona kesho kwa jicho au mtazamo wa mafanikio.

Ikiwa utaona kesho njema kwa ajili yako basi ndivyo itakavyokuwa kwani kila kitu kinaanza kwanza kwenye fikra zako.

Epuka kauli kama vile mimi ni maskini, mimi ni wa kuachwa au mimi ni wakufa tu.

7. Jitahidi Kuwa na Shukurani Kwenye Maisha

Ni vyema ukawa mtu mwenye shukurani kwa ajili ya watu na maisha. Kuwa na shukurani kutakuwezesha kupokea mengi zaidi kesho kuliko ungekuwa mtu wa kulalamika na kulaumu.

Ni vyema ukajifunza kushukuru hata kwa mambo madogo kwenye maisha yako. Kuna mtu anatamani kupata hata vile ulivyo navyo au kuwa kama wewe lakini hawezi.

Ni vyema kushukuru hata kwa kuwa na uhai na afya njema.

8. Jitahidi Kufanya Mambo Yaliyo na Umuhimu Kwako

Ni rahisi kupelekwa huku na huko na mambo mengi kwenye maisha. Hivyo ni vyema ukatambua maisha ni zaidi ya mambo kama vile kupata hela nyingi au umaarufu.

Ni lazima ufanye yale ambayo yana kuwezesha kufikia malengo na ndoto zako. Kama ni elimu basi tafuta elimu, kama ni maandalizi ya mazingira mengine basi yafanye.

Kama unataka kuboresha kesho yako basi epuka kufanya mambo kwa sababu mwingine anafanya ni lazima ukumbuke kuwa kuleta mabadiliko ni kufikiri na kuwa tofauti.

9. Jitahidi Kutenganisha Mambo Ya Ofice na Nyumbani

Hapa simaanishi kuwa usifanye chochote kiachohusiana na kazi yako nyumani, bali ujifunze kutenganisha ofisi na familia.

Kama unataka kuwa na kesho nzuri ni lazima ujifunze namna bora ya kuweka vipaumbele. Watu wengi wameshindwa kutofautisha nafasi ya kazi/ofisi na familia.

Wengi wamekuwa wakitumia muda wa familia kwa ajili ya kazi au wakitumia muda wa kazi kwa jili ya familia.

Nimeshuhudia watu wakikosa hata muda wa malezi ya watoto kwa kigezo tu kuwa wana kazi nyingi. Ni wazi kuwa ni lazima kila kimoja kiwe na nafasi yake ili uweze kujenga kesho njema yenye mpangilio na utulivu.

10. Jitahidi Kujifunza Kusamehe

Katika jambo ambalo limekuwa gumu kwa watu wengi ni kusamehe na kusahau wale waliowakosea. Kumbuka kuwa kubeba maumivu na uchungu moyoni mwako hakutakuwezesha kuwa na kesho njema bali mbaya.

Ni lazima ujaze nafsi na moyo wako furaha inayopatikana baada ya kusamehe; kwani kutosamehe kunaweza kusimuathiri aliyekukosea bali kukakuathiri wewe mwenyewe.

11. Jitahidi Kupumzika na Kuburudika

Ni vyema ukafahamu kuwa kesho yako inategemea afya njema ya mwili na akili. Hivyo ni vyema ukatenga muda wa kutosha kwa ajili ya kupumzika na kuburudika.

Kwa kufanya hivi mwili wako na akili vitajijenga na kujisafi kwa ajili ya kuanza kesho nzuri yenye tija na furaha.

12. Jitahidi Kusahau Mambo Yaliyopita

Kuna usemi usemao “Yaliyopita si ndwele tugange yajayo”. Ni vyema ukajifunza kutoruhusu zamani yako kukushikilia kusonga mbele kuelekea kwenye kesho yako yenye mafanikio.

Kumbuka kuwa huwezi kubadili jana wa juzi lakini unaweza kubadili kesho na kesho kutwa. Fanya yale yanayowezekana kubadili kesho yako na kamwe usiruhusu kurudishwa nyuma na kale yako.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo