Jinsi Ya Kufuga Kuku wa Kienyeji na Faida zake Tanzania

Ufugaji ni mzuri na pia faida za ufugaji wa kuku ni nyingi sana lakini katika ufugaji wa kuku inakubidi ufuate njia nzuri za ufugaji ili uweze kupata faida katika ufugaji wako zifuatazo ni njia za ufugaji wa kuku Tanzania

A. Ufugaji za mfumo huria

Katika mfumo huu wa ufugaji wa kuku, kuku huachiwa wakitembea toka asubuhi wakijitafutia chakula na maji na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku.

Huu ni mfumo rahisi lakini si nzuri kwa ufugaji wa kuku wengi kwani utahitaji eneo kubwa la ardhi.

Faida 

Mfumo huu una faida za gharama ndogo za uendeshaji kiujumla.

Hasara

  • Uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, kuibiwa mitaani n.k
  • Kuku huweza kutaga popote na kusababisha upotevu mkubwa wa mayai.
  • Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa
  • Utagaji unakuwa si nzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Uwekaji kumbukumbu si nzuri.
  • Ni vigumu kugundua kuku wagonjwa hivyo kusababisha ugumu katika utoaji wa tiba.

Utumiaji nzuri wa mfumo huu

  • Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine wowote hali ya hewa inapokuwa si nzuri.
  • Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji.
  • Kuku waandaliwe kwa viota vya kutagia.

Kuku 100 ni vizuri wakitumia eneo la ardhi la ekari 1.

B. Ufugaji wa mfumo wa nusu huria

  • Huu ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa uzio/ wigo. Mfumo huu ni ghari kiasi ukilinganisha na mfumo huria lakini huweza kumpatia mfugaji faida haraka sana.

Faida

  • Sehemu ndogo ya ufugaji wa kuku hutumika kuliko ufugaji huria, utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na mfumo huria, Ni rahisi kutibu magonjwa ya mlipuko kama mdondo (Newcastle desease), Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo sana ukilinganisha na mfumo huria.

C. Ufugaji wa mfumo wa ndani

Kuku hujengewa banda rasmi na ufugaji wa kuku hufanywa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa.

Faida

  • Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku pia Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine.

Hasara

  • Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda

Utumiaji mzuri wa mfumo huu.

1. Matandiko yageuzwe kila siku

2. Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia.

Mita mraba moja hutosha kuku 5 hadi 8.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

23 Comments
  1. Naitwa THOMAS AMOS, nipo simiyu bariadi. Je, nikiwa na mtaji wa TZS 500,000 kwa ufugaji wa kuku 5 naweza kuwamudu kuwahudumia Hadi pale watakapoanza kutoa faida?

  2. Mimi Nina changamoto ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na ukuzaji wa vifaranga najitahidi sana lakini ukuaji wake ni washida sana kuku wangu ni wa kienyeji.

    • wafungie kwenye kibanda maalum afu wawekee taaa ya wats 100, wahakikishie maji safi na chakula watakuwa vizuru sana

    • Changamoto katika ufugaji wa kuku zipo nyingi sana Rafiki yangu ila usikate tamaaa pia jitahidi sana kujua wengine walifanyaje wakazishinda changamoto hizo pia jitahidi sana kujifunza kwa wengine pamoja kusoma vitu vipya vinavyo husiana na ufugaji wa kuku.

      Usikate tamaa katika ufugaji wowote ule kwasababu hata mimi pia nilieandika hii post bado kuna changamoto mpya nakutana nazo.

  3. Mimi nafanya ufugaji wa kuku wa kienyeji Nina Kuku wa kienyeji 30 ila tatizo kwenye msimu wa joto kali kuku wangu wanaanza kuumwa na nikinunua dawa unakuta dawa zingine haziponyeshi mpaka naamua kuwauza kuku bila mpangilio.

    • Pole sana Jaribu Kumwona daktari wa kuku wa kienyeji nazani atakushauri vizuri jinsi ya kufuga kuku wa kienyeji kwa kuendana na mazingira uliyopo ili uweze kupata faida katika ufugaji wako.

      kwasababu kuna uwezekano ikawa ni tatizo la kimazingira.

  4. Ninataka nianze kufuga kuku wa kienyeji Pamoja na kuku wa aina ya chotara Pia Nataka nianze ufugaji nikiwa na kuku 100.

    Je mnanishauri niwe na mtaji wa kiasi gani kabla sijajenga Banda La Ufugaji wa Kuku?

    • Kuhusu gharama ya kuhudumia Kuku inategemeana na vitu vingi sana ikiwemo Mahali ambapo unafanyia Ufugaji wako Je ni Ndani Ya Mji au Nnje ya Mji?

      Pia inategemea na nani ambaye anawahudumia hao kuku na Chakula unatengeneza mwenyewe au Unanunua? Haya Maswali yatakusaidia sana Kujua Makadilio ya Gharama ya Ufugaji utakayotumia.

  5. Nataka Kuanza Ujasiriamali wa Kufuga Kuku Je mnanishauri nianze na mtaji wa sh ngapi?

    • Kwa wajasiriamali wadogo na wakati Kwenye swala la Ufugaji wa Kuku napendaga kushauri ni vizuri ukaanza kidogo kidogo kulingana na ulichonacho.

      Hii itakufanya kupata uzoefu wa jinsi ya kupambana na changamoto katika ufugaji wa kuku.

  6. Mimi Nina mtaji wa laki 2 na ninahitaji kufuaga kuku pia idadi ya vifaranga ninavyopanga kuanza navyo ni zaidi ya 67.

    Je Kwa makadirio haya ni kiasi gani Cha pesa kitahitajika kuwatunza hao kuku?

    • Kuhusu gharama ya kuhudumia kuku inategemea na nani ambaye anawahudumia hao kuku na Chakula unatengeneza mwenyewe au Unanunua?

      Haya Maswali yatakusaidia sana Kujua Makadilio ya Gharama ya Ufugaji utakayotumia.

  7. Ok vizuri vipi kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai kuna changamoto gani na je ufugaji huu una faida?

  8. Asante kwa somo zuri la ufugaji wa kuku nimejifunza kitu kikubwa sana hapa.

  9. Natamani kuanza na mimi ufugaji wa kuku ila naogopa kweli kweli nifanyaje?

  10. Asante sana kwa somo hili nataka kuanza ufugaji wa kuku nimepata point wapi nianzie katika kuandaa ufugaji huu.

  11. Nimependa sana maelezo yako pia ni mikoa gani mizuri kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji?

Leave a Reply to Lenald Minja Cancel reply