Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Ya Uandishi Tanzania

Kama umewahi kuwa na ndoto au matamanio ya kuwa mwandishi mkubwa hata kuwa mwandishi bora katika blogu yako, basi ni vyema ukajifunza namna ya kuwa mwandishi bora.

1. Jitahidi Kusoma Maandiko Bora

Ni dhahiri kuwa ukihitaji kufahamu nini mana ya uandishi bora ni lazima usome maandiko bora yaliyoandikwa na waandishi mahiri.

Soma maandiko bora kadri uwezavyo kwani utajifunza mambo mbalimbali yakiwemo mpangilio wa hoja, uwasilishaji na matumizi ya lugha.

Kama una tatizo la kifedha unaweza kusoma maandiko mbalimbali yanayopatikana kwenye mtandao kwa gharama nafuu kabisa kuliko kununua vitabu au machapisho mengine.

2. Jitahidi Kujifunza Kanuni Bora za Uandishi

Uandishi una kanuni zake kama ilivyo kwa taaluma nyingine. Unatakiwa kufahamu maswala kama vile matumizi ya lugha, alama za uandishi, upangaji wa hoja na mbinu za uhariri.

Kwa kufanya hivi utaweza kuboresha uandishi wako na kuufanya kuwa wa kiwango cha juu kabisa.

3. Jitahidi Kuandika Sana

Kadri unavyoandika kwa wingi ndivyo unavyojenga uzoefu wako zaidi. Uzoefu hupatikana kwa kufanya jambo fulani kwa muda mrefu.

Hivyo jitahidi kuandika maandiko/matini mengi kadri uwezavyo ili uweze kunoa uwezo wako wa uandishi Kupitia mbinu hii utaweza kubaini changamoto mbalimbali za kiuandishi na njia ya kuzitatua.

4. Jitahidi Kutenga Muda Bora wa Kuandika

Siyo wakati wote unafaa kwa ajili ya shughuli za uandishi. Ni vyema ukajitengea muda ambao uko vyema kiafya na kiakili.

Mara nyingi asubuhi ndipo mtu anapokuwa na nguvu za kimwili na kiakili kufanya kazi mbalimbali. Hivyo ni vyema ukabainisha muda ambao wewe mwenyewe unaona ni bora kwako kufanya shughuli za uandishi bila matatizo.

5. Jitahidi Kuondoa Vitu Vinavyokuvuruga

Maisha yetu yamejaa vitu mbalimbali. Vingine hutawala sehemu kubwa ya maisha yetu kiasi cha kutaka kuingilia au kuvuruga kila tunachokifanya.

Ili kuwa na ufanisi katika uandishi ni vyema ukaodoa vitu mbalimbali vinavyoweza kukuvuruga kama vile mitandao ya kijamii, simu, televisheni, michezo ya kielektroniki, watu.

Unaweza kuzima simu au data katika vifaa vyako ili kuzuia kuvurugwa na mambo ya mtandao. Unaweza kutafuta chumba au eneo maalumu lenye utulivu litakalokuruhusu kufanya kazi yako ya uandishi kwa utulivu.

Kwa mfano ninapoandika makala hii nimekaa katika chumba cha kusomea ili kuhakikisha ninapata utulivu wa kutosha.

6. Jitahidi Kuorodhesha Mawazo

Ni jambo zuri ukajizoesha kuorodhesha mawazo kabla ya kuanza kuandika. Kwa kufanya hivi utakuwa umejiwekea mwongozo mdogo utakao kuongoza juu ya yale unayoyandikia.

Unaweza kutumia kipande cha karatasi, shajara, au hata programu za kompyuta kama vile MS Word na Google Docs ili kuorodhesha mawazo yako.

7. Jitahidi Kuandika Bila Kuacha

Ni vigumu kujikita katika uandishi bila kuacha kama hujajiwekea lengo na kuwa na mtindo anuwai wa uandishi.

Ni dhahiri utazamapo karatasi nyeupe au ukurasa mweupe kwenye kompyuta unaweza ukasita au ukakata tamaa ya kuandika mapema. Hivyo, unaweza kufanya haya yafuatayao ili kuweza kuandika bila kuacha.

  • Andika tu mawazo kadri yanavyokuja akilini mwako kwani utayahariri baadaye.
  • Usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja; yaani jikite tu kwenye kuandika bila kujihusisha na mambo mengine.
  • Usihariri; unapohariri wakati unaandika utapunguza ufanisi katika uandishi wako. Andika kwanza na utahariri baadaye.

Ukitumia mbinu hii utaweza kuandika mambo mengi kwa muda mfupi kwa urahisi zaidi bila kuacha au kukata tamaa.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo