Hasara za Kuangalia Tv Kwenye Maisha

Televisheni imekuwa ni kifaa muhimu kwa ajili ya habari na burudani Tanzania hata hivyo television inaweza kuwa na madhara kadha wa kadha kwako ikiwa haitotawaliwa vyema.

1. Kuangalia Tv Hupoteza Muda

Unapokaa na kuangalia televisheni ni wazi kuwa unatumia muda mwingi na wa muhimu sana. Hii ni kutokana na sababu kuwa watu wengi hutazama televisheni kwa muda mrefu au hata siku nzima.

Utazamaji wa televisheni wa muda mrefu unaweza kukupotezea muda mwingi ambao ungeweza kuutumia kufanya kazi nyingine hasa zile zinazokuongezea kipato na maarifa.

2. Kuangalia Tv Huaribu Mahusiano

Unapokaa muda mrefu kwenye televisheni ni wazi kuwa utajitenga na watu wengi. Hutopata muda wa kushirikishana hili au lile na watu wengine wala kuwasaidia wale wanaohitaji msaada wako.

Kukaa karibu na watu wengine kwenye jamii hukufundisha mambo mbalimbali pamoja na kuboresha mahusiano yako ya kijamii. Hili ni tofauti na kukaa mbele ya televisheni siku nzima ukitazama filamu au mziki.

3. Kuangalia Tv Hupoteza Pesa

Chaneli bora za televisheni zinapatikana kwa gharama kubwa; ikizingatiwa pia televisheni huhitaji umeme ili iweze kujiendesha, hili pia litaendelea kukugharimu fedha.

Ikiwa wewe unapenda kutazama televisheni sana, utatumia fedha nyingi kwa ajili ya kukidhi kile unachokipenda. Hata hivyo, ungeweza kuzitumia pesa hizi kwa kuwekeza, kuweka akiba au kufanya kitu kingine chenye tija zaidi kwako.

4. Kuangalia Tv Taarifa za Uongo

Siyo taarifa zote au vitu vyote vinavyoonekana kwenye televisheni ni vya kweli. Hivyo kutazama na kuiamini sana televisheni kunaweza kukusababishia kupata taarifa za uwongo.

Watu wengi unaowaona kwenye televisheni huishi maisha ya mbele ya kamera yaani maisha ambayo siyo halisi hivyo pia kuiga maisha haya kunaweza pia kukupoteza.

5. Kuangalia Tv Huathiri Afya

Binadamu hatakiwi akae kwa muda mrefu sana; hivyo kwa wale wanaokaa kwenye televisheni muda mrefu sana au hata siku nzima, hawazitendei haki afya zao.

Ni muhimu kufanya kazi za kuuchangamsha mwili au kufanya mazoezi mara kwa mara ili kulinda afya yako kuliko kukaa tu mbele ya televisheni.

Ikumbukwe pia tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa televisheni ni chanzo kikubwa cha ongezeko la unene kwa watu wengi duniani.

6. Kuangalia Tv Hupoteza Usingizi

Watu wengi hukosa usingizi kwa sababu ya kukesha wakitazama televisheni. Usingizi wa kutosha ni swala muhimu sana kwa ajili ya afya ya mwili na akili yako.

Usingizi bora utakuongezea pia ufanisi katika yale unayoyafanya.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

2 Comments
  1. Mbarikiwe nimejifunza kitu kikubwa sana kuhusu madhara ya hizi Tv.

Leave a reply

Wauzaji
Logo