
Faida za ufugaji wa kuku ni nyingi lakini leo nitaelezea faida na hasara za ufugaji wa kuku wa kisasa, kienyeji ambazo kwa wengine huenda zikawa ni ngeni kwao ;
- Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa kienyeji linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba mbadala)
- Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele (shampoo)
- Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
Jinsi ya kupata faida katika ufugaji wa kuku
- Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka
- Zuia viroboto, utitiri na minyoo.
- Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
- Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
- Kula mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
- Kipato unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku
Hasara katika ufugaji kuku
- Yako mapungufu mengi yanayofahamika lakini hapa naomba niweke lile la muhimu zaidi. Magonjwa ya kuku kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku kutokana na kutokuzingatia kuchanja kuku kwa wakati.