
Kusikiliza muziki ni jambo zuri sana maishani na watu wengi Tanzania wanapenda kusikiliza muziki na Tafiti zinabainisha kuwa kusikiliza mziki kuna manufaa mengi kwa ajili ya afya ya mwili na akili.
1. Mziki Hutufanya Tuwe na Furaha
William James alsisema “Siimbi kwa sababu ninafuraha, bali nafurahi kwa kuwa ninaimba” .
Kusikiliza mziki huzalisha kemikali ya dopamane ambayo hutufanya tujisikie vizuri. Hii ndiyo sababu mtu akiwa anajisikia vibaya au kukosa furaha mara nyingi anaposikiliza mziki hasa wa taratibu hujisikia vizuri.
Hivyo basi, wakati ukiwa umekosa raha unaweza kusikiliza nyimbo unazozipenda angalau kwa dakika 15 ili kukuweka katika hali nzuri zaidi.
2. Mziki Huongeza Ufanisi Katika Kukimbia
Mtafiti Marcelo Bigliassi na wenzake walibaini kuwa wakimbiaji wanaosikiliza mziki walimaliza mbio za mita 800 haraka zaidi kuliko wengine.
Hivyo ni dhahiri kuwa kusikiliza mziki wakati wa kukimbia kunaweza kuwa kama hamasa zaidi. Unaweza kusikiliza mziki wa haraka haraka au taratibu kulingana na vile unavyopendelea.
3. Mziki Huondoa Msongo na Kuboresha Afya
Kusikiliza mziki hupunguza kwa asilimia 60 homoni zinazosababisha msong stress. Ikiwa basi msongo utapungua ni dhahiri kuwa pia maradhi mengi ambayo chanzo chake ni msongo yatapungua kama si kwisha kabisa.
Unaweza kusikiliza mziki na kuimba wakati mziki unapoimba; pia usisahau kucheza angalau kwa kuchezesha mguu ili kupata tiba hii kamili.
4. Mziki Hutusaidia Kulala Vizuri
Kusikiliza mziki husafisha ubongo wako na kuuweka katika hali nzuri itakayokuwezesha kupata usingizi mzuri.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini ukisikiliza mziki wa taratibu mara nyingi unapatwa na usingizi? Ni dhahiri kuwa mziki una nafasi kubwa katika kulala kwetu.
Inashauriwa wakati wa usiku kuweka ubongo wako katika hali nzuri ili uweze kulala vyema; unaweza kusikiliza mziki wa taratibu kabla ya kulala.
5. Mziki hukuweka katika hali nzuri unapoendesha gari
Wakati mwingine kuendesha gari ni kazi inayochosha; hivyo inahitaji kiburudisho ili kuifanya vyema. Ni dhahiri kuwa madereva wanaoendesha magari masafa marefu hupenda kusikiliza mziki ili kujiweka katika hali nzuri.
Hivyo baisi, unaweza kusikiliza mziki unapoendesha gari. Kumbuka kuzingatia sheria za barabarani; usisikilize kwa sauti kali kiasi cha kushindwa kusikia sauti nyingine barabarani kama vile honi ili kuepuka ajali.
6. Mziki Hutuwezesha Kujifunza
Baadhi ya watu wamebainisha kuwa wanaposoma au kujifunza mambo kadhaa wakati wakisikiliza mziki, basi hufanikiwa kuyamudu maswala hayo vyema.
Si jambo la kustaajabisha kuwaona watu wakisikiliza mziki huku wakisoma vitabu, majarida, tovuti nk. Hata hivyo, hili linategemea mtu na mtu, wengine hawapendi kusoma au kujifunza huku wakisikiliza mziki, wakati wengine hupenda kufanya hivyo.
Hivyo uamuzi ni wako kuwa unapenda mziki au laa; na ni mziki wa namna gani unaopenda wakati wa kusoma na kujifunza.
7. Mziki Hupunguza Maumivu
Pia utafiti uliofanyika katika chuo cha Drexel cha Philadelphia ulibaini kuwa mziki wa taratibu au wa jadi, hupunguza maumivu kwa wagonjwa wa saratani pamoja na wale walioko katika kitengo cha uangalizi maalumu (ICU).
8. Mziki Hutuhamasisha
Wakati mwingine unakata tamaa au unakutana na mawimbi mengi sana maishani kiasi cha kuzidiwa. Ni dhahiri ipo miziki inayotia watu moyo na kuwahamasisha.
Ipo mifano ya watu wengi waliotaka kujiua lakini baada ya kusikiliza miziki inayowaeleza umuhimu wa kuendelea mbele na maisha walisitisha mpango wao.
Hivyo kusikiliza mziki kunaweza kukuhamasisha kuendelea kutoka ngazi moja hadi nyingine.
9. Mziki Hutukumbusha Mambo
Ni dhahiri kuwa miziki mingi huambatana na matukio au vipindi fulani vywa muda. Si jambo la kustajabisha ukasikia mziki fulani ukakukumbusha matukio au eneo fulani ulilokuwa zamani.
Watu wamekuwa wakikumbushwa matukio ya furaha kama vile ndoa, mahafali, au hata ya uzuni kama vile misiba na maradhi.
Hivyo ni wazi kuwa kwa njia ya mziki tunaweza kukumbuka matukio au watu fulani tuliowahi kukutana nao maishani mwetu.
Kabisa mziki ni tiba mbadala ya dawa. Thank you nimejifunza kitu kuhusu hizi faida za kusikiliza muziki.
Asante sana Martin kwa comment yako na mimi nimefurahi kusikia hivyo.