Faida za Kupanga Bajeti Kwenye Biashara

Faida na umuhimu wa kupanga bajeti ya biashara yako Tanzania pamoja na manufaa ya kupanga bajeti kwenye maisha ya kila siku kwa ujumla.

1. Utaelewa Fedha Zako Mahali Zinapo kwenda

Ukiwa hauna bajeti na unaingiza kipato kila siku au kila mwezi unaweza ukawa unapata pesa nzuri sana lakini ukawa huelewi fedha zinaenda wapi au umezifanyia kazi gani, kwani utajikuta unafanya manunuzi ya vitu ambavyo sio mahitaji yako muhimu.

Bajeti itatenga kila fedha unayo ipata ifanye kazi gani au uifanyie manunuzi gani na sio unakurupuka kununua nunua vitu bila kuwa na mpangilio, lakini pia utapata kuelewa mahitaji yako kwa siku ni kiasi gani na kukupa motisha ya kuongeza kipato chako kwa siku. 

2. Itakuepusha na Hatari Ya Kufilisika

Ukiwa na tabia ya Kuweka bajeti ya matumizi ya pesa Kila Siku moja ya jambo utakalo epuka nalo ni pamoja na kuepuka kufilisika kwani unapoifuata bajeti unaepuka kutumia pesa zaidi ya ile unayo ipata.

3. Husaidia Kuepukana Na Madeni

Ukiwa na bajeti itakusaidia kununua vitu kwa kwa cash na pia ukiwa na bajeti pesa yako unao uwezo wa kuweka akiba ya kipato unacho kipata Kila siku.

Bajeti itakusaidia kubana matumizi ya pesa yasio rasmi.

4. Husaidia Kuepuka na Matumizi Makubwa Ya Pesa

Bajeti hukupatia mwongozo wa kufuata kipi ununue na kipi usinunue kwa wakati huo kwani kiasi kilichopangwa kwa siku, wiki au mwezi ndicho kitakacho kukuruhusu au kutokuruhusu kufanya manunuzi.

5. Inasaidia Kutimiza Malengo ya Muda Mrefu

Bajeti kama mwongozo wa matumizi ya Pesa au Kipato chako, itakusaidia sana pale ukiwa na malengo ya nunua au kuanzisha Kitu flani kikubwa.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general