Faida za Kuanzisha Biashara Ukiwa na Umri Mdogo

Faida na umuhimu wa kuanza kuanzisha Biashara Tanzania ukiwa bado na umri mdogo pamoja na mtaji kidogo.

1. Utapata Uzoefu wa Biashara

Mtu ili upate uzoefu wa jambo lolote lazima uwe umefanya jambo hilo kwa muda flani angalau miaka mitatu na kuendelea. 

Pia hata Katika Biashara yoyote ukiwa umesha wahi kuifanya kuna mambo mengi utakuwa umejifunza ikiwemo changamoto za Biashara, mbinu za Kibiashara na Njia bora ya Huduma kwa wateja.

2. Kujipima Uwezo Wako wa Mbinu za Biashara

Ukiwa unafanya Biashara utapitia changamoto na vipindi tofauti tofauti hivyo Ufanyaji wa Biashara ukiwa bado mdogo utajipima mwenyewe kujua uwezo wako wa ushawishi kwa wateja na namna ya Kutatua changamoto za Kibiashara.

3. Utajifunza Kanuni za Pesa

Katika Biashara yoyote Unaweza kuwa unapata wateja wa kutosha na faida kubwa lakini ukashindwa namna ya kuifanya Pesa hiyo izae Pesa zingine nyingi zaidi kwani unaweza kujikuta unakuwa na matumizi makubwa binafsi mpaka unakula mtaji. 

Bajeti katika mapato na matumizi ni muhimu ili kulinda Mtaji na Biashara yako.

4. Utapata Nidhamu Ya Biashara

Tunapo sema Nidhamu ya Biashara namaanisha kuheshimu Biashara yako au kwa lugha nyingine naweza sema Kuendana na Biashara yako.

Mfano kama Biashara yako inakuhitaji ufungue ofisi yako Saa mbili Asubuhi hakikisha unaheshimu huo mda kwani Boss ni wewe mwenyewe.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general