Faida Ya Mbolea za Asili

Mbolea za asili ni nzuri na kuna Faida za matumizi ya mbolea za mboji katika kilimo cha mazao mbali mbali na zifuatzano ni baadhi ya faida za mbolea za asili.

Faida za Mbolea

  1. Utengenezaji wa mbolea ya mboji hauna gharama na ni rahisi hivyo wakulima wa ngazi zote wanaweza kuumudu.
  2. Mbolea ya mboji huboresha muundo wa udongo unaopelekea kuwa na mzunguko mzuri wa hewa na maji katika udongo.
  3. Mbolea ya mboji huongeza virutubisho vinavyohitajika na mmea katika udongo na hivyo kuongeza mazao.
  4. Mboji huongeza uwezo wa udongo kutunza maji na hivyo kupunguza kasi ya ukaukaji wa udongo hasa katika maeneo yenye hali ya joto na yasiyopata mvua za kutosha.
  5. Mbolea ya mboji huweza kutumika kama mbadala wa mbolea ya samadi wakati wakuandaa kitalu cha mboga.
  6. Mbolea ya mboji huboresha afya ya mmea na kufanya uwe na uwezo wa kustahimili magonjwa.
Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply

Wauzaji
Logo