Biashara za Mtandaoni zenye Faida Kwa Tanzania

Biashara za mtandaoni zinazoingiza pesa

  • Biashara Ya Kuanzisha Tovuti

Kuna tovuti chache sana zilizopo kwa lugha ya kiswahili na hiyo peke yake ni fursa tosha kwako kuanzisha tovuti na kutengeneza kipato.

Kama unafikiria kufanya hivi ni muhimu kuhakikisha kuwa unajua nini hasWa wasomaji wako wanataka kukipata katika tovuti yako.

Weka jitihada kubwa katika kuwafikia wasomaji wengi katika tovuti yako mtandaoni na kuwa na idadi inayoridhisha ili kuvutia matangazo kutoka kwa wadau mbalimbali.

  • Biashara Ya Utafutaji masoko kwa niaba ya makampuni (Affiliate Marketing)

Japokuwa ni vigumu kwa kampuni kukosa kitengo cha masoko bado kuna fursa nzuri ya kujiajiri kutafuta matangazo kwa ajili ya makampuni mbalimbali ikiwa una idadi kubwa ya wafuatiaji na ushawishi wako mtandaoni na katika jamii ni mkubwa.

Ikiwa una vitu hivyo basi unaweza kugeuza ushawishi wako kama ajira kwa kutafuta wateja kwa ajili ya makampuni.

Jambo la muhimu katika ajira hii ni kuhakikisha kuwa unakuwa uaminifu na unawasaidia wateja kuelewa bidhaa kwa undani.

Unapojenga mahusiano mazuri na ya muda mrefu na wafuatiaji/wateja wako, inakuwa rahisi kuwauzia bidhaa au huduma mbalimbali.

  • Biashara Ya Dropshipping

Hakuna neno rasmi la kiswahili la biashara hii lakini kwa ufupi Dopshipping ni kitendo cha kuwanunua wateja bidhaa mtandaoni.

Ikiwa wewe ni mfanyabiashara ambaye kwa asilimia kubwa unategemea mitandao bila shaka umewahi kukutana na watu wanaofanya biashara hii kwa kuwa wafanyabiashara walio wengi wanakutana na vikwazo kama njia rahisi za malipo na usafirishaji hali inayowafanya kushindwa kuagiza bidhaa wenyewe moja kwa moja.

Unaweza kununua bidhaa moja kwa moja katika mitandao kama Amazon na Ebay na kuhakikisha mzigo unamfikia mteja moja kwa moja pasipo yeye kuwasiliana na kampuni husika.

Biashara hii inahitaji uaminufu wa hali ya juu pamoja na jitihada za kufanya kazi bila kuchoka hususani kama ndio kwanza unaanza.

  • Biashara Ya Kuanzisha Youtube Channel

Sawa na kuanzisha tovuti kabla hufungua chaneli yako ya Youtube ni muhimu kujua ni nini hasa unataka kufanya kwani itakusaidia kujipanga vizuri zaidi.

Watu wengi hushindwa katika hili kutokana na kukosa muelekeo sahihi na hivyo kupoteza wafuatiliaji kirahisi. Ni muhimu kuwa na mpango ambao utakuongoza na kukusaidia kufanikisha malengo yako.

Youtube imesaidia watu wengi kujiajiri na kutengeneza kipato cha uhakika hivyo ni kiyu ambacho kinawezekana kabisa ukijipanga vizuri na kufanya kazi kwa bidii.

  • Social Media Influencer

Ikiwa wewe ni mtumiaji mkubwa wa mitandao ya kijamii na una idadi nzuri wa wafuatiliaji basi unaweza kutumia njia hiyo kujiingizia kipato kwa kushirikiana na makampuni makubwa kutangaza bidhaa au huduma wanayotoa.

Pamoja na hayo unaweza kutumia ukurasa wako kwa ajili ya matangazo na kutengeneza kipato kizuri Vijana wengi wameendelea kujiajiri kwa kupitia mitandao kama Instagram.

Ikiwa una idadi kubwa ya wafuatiliaji hii ni fursa nzuri kwako kutengeneza fedha na kufanya kazi na biashara mbalimbali.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

12 Comments
  1. Nimezipenda sana hizi biashara nitaanza kuzifuatilia au wewe unanishauri ipi ni nzuri zaidi mtandaoni?

  2. Asante sana nimefurahi kwasababu Napenda sana Nianzishe Biashara za Mtandaoni Je faida zake ni kubwa?

    • Biashara nyingi za Mtandaoni siku zote faida yake inaanza ikiwa ndogo sana ila kila siku biashara inavyokuwa na faida inazidi kupanda.

      Hivyo basi Online Business mara nyingi Siku za Mwanzoni huwa inahitaji sana uvumilivu na moyo wa kujitoa.

  3. Na mimi nitaanza kufanya biashara online

  4. Asante biashara nimezipenda kabisa.

  5. Nazipenda sana biashara za mtandaoni na mimi natamani siku niweze kufungua hata youtube channel yangu

  6. Maelezo mazuri sana na mimi nitachagua biashara moja wapo ya mtandaoni nikazane nayo.

Leave a Reply to Lenald Minja Cancel reply