Biashara za Kufanya Maeneo Ya Chuo

Biashara zinazolipa na zenye faida ambazo unaweza kuzifanya ukiwa karibu na maeneo ya chuo kwa hapa Tanzania.

1. Biashara Ya Nyumba Za Kupanga

Makazi ni hitaji muhimu sana kwa binadamu, hivyo sehemu ya vyuo wanafunzi watahitaji vyumba kwa ajiri ya kuishi pia wafanyakazi wa chuo nao ni mateja wa vyumba vya kupanga.

2. Biashara Ya Vifaa Vya Kielekitroniki

Vifaa vya kielekitroniki ni pamoja na simu za mkononi, computer, chargers, usb, covers za simu, screen protector, betri za pc au laptops na vingine vingi vitumiavyo umeme ambavyo ni moja ya mahitaji ya wanafunzi. 

3. Biashara Ya Vyakula

Ulaji ni hitaji muhimu sana kwa kiumbe hai chochote kwa hiyo katika mazingira au taasisi ya kielimu kama chuo wanafunzi na wafanya kazi wanahitaji hii huduma muhimu sana.

Kwenye swala la chakula jitahidi usafi na ubora wa chakula kwani unaweza kupoteza wateja kwakuwa na huduma mbaya.

4. Biashara Ya Nguo Na Mabegi

hapa nimejumuisha yale maduka ya kuuza nguo tofauti tofauti. kuvaa ni jambo la muhimu kwa binadamu hivyo ukiwa na duka la nguo kuendana na mazingira ya chuo. 

5. Biashara Ya Saloon

Saloon yaweza kuwa ya Kike au Kiume, katika saloon yako jitahidi Kujidhi mahitaji ya wanafunzi na kuendana na Mitindo ya Kusuka au kunyoa.

Pia zingatia eneo la saloon yako, hakikisha inaonekana na Kufikika kiurahisi na Katika Saloon ya Kike unaweza Kuuza Rasta yaani Nywele za Kusukia kwa Wadada.

6. Biashara Ya Huduma za Stationery

Uhitaji wa huduma za Stationary ni mkubwa sana kwani watahitaji kutoa photoCopy, Passport size, Kuprint, typing, Handouts, lamination  na huduma nyingine nyingi zifananazo na hizo.

7. Biashara Ya Huduma za Kifedha

Huduma ya Kifedha ni Muhimu sana, kwani katika Mazingira ya Vyuoni wanafunzi wengi Hupokea na kutuma Pesa Kutoka Nyumbani au sehemu zingine.

Pia kwa Vyuo Vikuu kwa wanafunzi wenye Mikopo pindi wakipokea Pesa ya kujikimu huwatumia wazazi na ndugu Pesa japo Kidogo.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply