Biashara Ya Vifaa Vya Ujenzi Tanzania

Biashara Ya Vifaa vya ujenzi tanzania ni nzuri sana lakini ili kufanikiwa katika biashara ya vifaa vya ujenzi kuna kuhitaji ujue mbinu za biashara pamoja na faida zake kwa tanzania

1. Litambue soko lako la Biashara Ya Vifaa

Kulitambua soko ni pamoja na kutambua wateja tarajiwa wa vifaa vya ujenzi na mambo wanayoyazingatia kabla hawajafanya maamuzi ya kununua. Kutambua bei zilizopo kwenye maduka mengine ya vifaa vya ujenzi katika eneo husika.

Hebu jiulize una madhaifu gani ambayo yanaweza kukufanya usifanikiwe katika biashara hii ya vifaa? Tafakari jinsi gani utapambana na madhaifu yako ili yasije kukupelekea ukapoteza biashara.

Tafakari key success factors za kufanikiwa katika biashara yako katika eneo ulipo. Katika eneo unalotarajia kufungua duka lalo la hardware kuna maduka mangapi mengine ya hardware?

2. Weka mikakakati makini ya kudhibiti ushindani wa Biashara

Weka mazingira mazuri ya mteja kujisikia raha anapofanya biashara na wewe kwa:

  • kutoa punguzo kwa baadhi ya bidhaa.
  • Kuweka njia nyepesi za mtu kutoa oda na kufikishiwa alipo pia humfanya mteja kujiskia raha kufanya biashara na wewe.

Hivi ungejiskiaje kama kila bidhaa ya vifaa vya ujenzi unayoitaka ingekua unaipata kwa kubofya vitufe kadhaa vya simu yako?

  • Basi hakikisha unawapa watu njia rahisi ya kuipata bidhaa ili waone tofauti kati yako na washindani wako.
  • Pia hakikisha kuwa duka lako la vifaa linakuwa ni one stop shop kwa maana kuwa bidhaa muhimu zote zinapatikana.

3. Ni bidhaa zipi za Vifaa Vya Ujenzi hutoka kwa kasi?

Hili ni swali muhimu lazima ulipatie jibu na Mara nyingi bidhaa zinazotembea kwa kasi ni pamoja na cement, steel bars, steel rods, misumari, white cement, vitasa, tiles za sakafuni na mabafuni, welding rods, vifaa vya plumbing. Ni vyema ukatazama vifaa vinavyotembea kwa kasi kwa kufanya utafiti kwenye maduka yaliyopo maeneo husika.

4. Masoko Ya Vifaa Vya Ujenzi

Usikae na kusubiri wateja wa vifaa waje dukani. Ushindani ni mkubwa sana Jaribu kuwa karibu na mafundi wa ujenzi na uwape commision kwa kununua kwako. Wafanye wawe na kila sababu ya kuagiza vifaa kwako.

Pia unaweza kuajiri kijana ambae kazi yake itakua ni kuzunguuka kuangalia maeneo ambayo watu ndio wanaanza kuchimba misingi na kuanza kujenga.

Kutembelea sehemu zinazojengwa itasaidia kuweka mahusiano mazuri na mafundi na wenye nyumba. Kumbuka ukienda sehemu zinazojengwa lazima utaulizwa bei za vitu muhimu kama cement, mabati etc. Jiandae uwe na bei nzuri na kama anaeuliza ni fundi muahidi commision kwa kununua kwako.

Hata kama awamu za kwanza kwanza utamuuzia kwa bei isiyokuwa na faida wala hasara ila mahusiano yenu yataimarika na kujipatia uhakika wa soko na hatimae kuongeza bei polepole.

Kumbuka pia unaweza uza kwa hasara bidhaa moja na bidhaa nyengine ukauza kwa bei ambayo inafidia ile hasara na kupata faida.

5. Usimamizi wa duka lako la Vifaa

Kama kuna kazi nyengine inakufanya uwe busy basi kuwa tayari kutumia muda kiasi nyakati za jioni ili kupitia mauzo na mwenendo wa biashara. Hesabu bidhaa kila baada ya mwezi kuhakiki kuwa kilichopo kina balance ukihusianisha kilichonunuliwa na kilichouzwa.

6. Makadirio ya gharama za Biashara Yako

Utahitaji walau 10m za kununulia mzigo wa kuanzia. Utahitaji pia walau 1.8m kwa ajili ya kodi kutegemeana na sehemu unapofungua duka lako. Utahitaji leseni na ikiwezekana usajili wa BRELA Utahitaji TIN kutoka TRA Na mahitaji mengine kadhaa.

Makadirio ya mtaji wa chini kabisa wa duka la vifaa vya ujenzi lenye mzunguuko mzuri na faida nzuri ni walau 15m.

Kwa kawaida kwenye biashara ya vifaa vya ujenzi kama utauza bidhaa za 10m kila mwezi utajipatia walau 750,000 kama faida. Hii ni sawa na 7.5%. Kazi ni kwako kuhakikisha unauza bidhaa nyingi zaidi kwa mwezi.

Tuandikie Email Yako Uweze Kupata Post za Wauzaji wa Tanzania Kwa Haraka.

6 Comments
  1. Nilikuwa nawaza kufungua biashara ndogo ya mtaji mdogo wa vifaa vya ujenzi asanteni sana wauzaji kwa kunipa muongozo huu.

  2. Asante sana Nimepata Mwangaza kuhusu biashara Hii ya vifaa vya ujenzi naamini nitafanyia kazi ili na mimi nianzishe hii biashara.

  3. Ahsanteni sana kwa muongozo huu. mnatusaidia sana sisi tunaoanzisha biashara hasa kwa mitaji midogo

Leave a reply

Wauzaji
Logo
Enable registration in settings - general