Biashara Ndogo Ndogo Zenye Mtaji Kidogo Tanzania

Biashara ndogondogo zenye faida kubwa tanzania na ambazo zinalipa na pia zinazohitaji mtaji kidogo ili kuanzisha pamoja na kuiendesha ukiwa tanzania

1. Biashara ya juice za matunda


Biashara ya Juice ya Matunda ya elfu kumi inaweza toa had lita kumi za juice ambapo lita moja ni sawa na glass tano au nne za juice so kwenye lita kumi upata grass 40 sawa na elfu ishirin ukitoa matunda, sukar na vigras unafaida elfu tano

2. Biashara ya matunda


Biashara ya matunda Siku hzi watu wengi hasa maofisini wanapenda kula matunda andaa kwa usafi matunda yako hapa unaweza tumia elfu kumi na tano.


Unanunua matunda mchanganyiko, nunua vifungashio vile vya kuwekea matunda pack matunda yako ambapo yakiuzika na biashara ikaenda vyema unaondoka na faida nusu kwa nusu

3. Biashara ya mkaa


Kwenye biashara ya Gunia la elfu 30 unaweza kutoa mafungu 45 ya mkaa sawa na elfu arobain na tano faida elfu kumi na tano


4. Biashara ya mobile genge


Biashara ya genge linalotembea unaweza kutumia smartphone kutangaza unauza vitu vya gengeni kama nyanya, vitunguu karoti, na vitu vingine ya jikoni, ukipata order unaenda ilala soko la wakulima unajumua vya kutosha unapeleka faida hapa ni nusu kwa nusu, pia unaweza tembezea majirani zako kutegemeanana sehemu unayoishi


5. Biashara ya bites


Biashara ya bites kama crips sambusa, chapati, maandazi, mihogo ya kukaanga, vitumbua karanga za mayai, ubuyu, korosho, visheti na bites zingine unaweza kufanya biashara ya kusambaza vitafunwa maofisini kwa package au ukauzia nyumbani moja ya vitafunwa hivyo


6. Biashara ya vinywaji baridi stend za daladala


biashara ya vinywaji Unaweza ukauza hata kwenye ndoo kama huna deli nunua mabarafu nunua vinywaji tafuta kijana au wewe mwenyewe uza biashara yako kwenye stend za daladala inalipa saaana


7. Biashara ya uji wa ulezi na uji wa Mchele


Biashara ya uji wa mchele pamoja na uji wa ulezi ni biashara nzuri sana unaweza kuanza kwa kuKodi toroli jaza chupa zako uji aina hizo tembeza kwenye magereji na sehemu za bodaboda.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

4 Comments
  1. Nimependa sana somo hili la biashara ndogondogo lakini inabidi muongeze na List za biashara zingine Kama vile vocha pamoja na M-Pesa.

  2. Asante Sana kwa hili somo lenu kuhusu biashara zuri mno.

Leave a Reply to Lenald Minja Cancel reply